Freeman Mbowe: Dar es Salaam kuna kikosi kazi cha utekaji
Wengi wanateteta kuwa sio Samia bali vijakazi wake ila wazungu husema 'Silence means consent', ukimya daima huchukuliwa kuwa ni ridhaa. Samia yupo kimya kuashiria ameridhia haya yote yatokee.

Kwa kila ovu linalofanyika nchini kwa sasa, ni kwa ridhaa ya Samia.
Umemaliza yote mkuu wangu. Yote ni maagizo toka No 1 mwenyewe.
 
“Kama Chama tumechunguza kutoka vyanzo vyetu vya ndani na vingine vya ndani ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, nitaeleza kwa kifupi tulichogundua na tunaowaonyooshea vidole ili Polisi na hao wengine watusute watuambie Mbowe mnasema uongo, uchunguzi wetu unatupeleka wapi? moja kuna kitu kwenye Kanda Maalum ya Dar es saalam kinaitwa Task Force ya Ulinzi na Usalama, Task Force hii iliundwa ikishirikisha Wadau kutoka Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na hata JWTZ, katika hatua ya baadaye Jeshi la Wananchi liliondoka katika oparesheni hii, na Task Force hii ilipoundwa kwa mara ya kwanza iliundwa kama Kikosi maalum cha kupambana na wizi ambacho kinasimamiwa na ZCO ambaye sasa hivi anayeongoza Ofisi hiyo anaitwa ASP Faustin Mafwele huyu ndio Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es salaam ambaye anasimamia Kikosi hiki”

“Oparesheni centre ya kikosi hiki ipo nyuma ya Kituo cha Polisi Chang’ombe na mtambue Kikosi hiki hakiingiliwi na mfumo wa kawaida wa utawala wa Polisi kwahiyo hakifanyi kazi ndani ya Vituo vya Polisi, nyuma ya Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kuna kambi ya Kikosi hiki na imezungushiwa uzio wa mabanzi pale ndani wanateswa Watu, wanaumizwa Watu, wanafinywa Watu pale ndio mateso ya Watanzania wanapopitia”

“Kwa taarifa tulizonazo kwa mwaka huu na sehemu ya mwaka jana, wapo Watanzania zaidi ya 200 hawajulikani walipo na mambo haya ni mwendelezo wa maelekezo ya Viongozi wa Serikali ambao huko nyuma walipaswa kusema shughulikeni nao”

Soma Pia: Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

“Sisi kama Chama tumesema tuyaseme haya kwa sauti ili yasikike zaidi, utekaji huu umeambatana na mauaji, awali waliokuwa wanauawa kienyeji walikuwa wanapelekwa mochwari, wengine kama Sativa walipelekwa pori la Katavi wakaliwe na Fisi kwasababu wanasema Katavi ndio pori lenye Fisi wakali ambao hata mfupa wanautafuna kama biskuti, Mungu hakupenda akamwokoa, Sativa alikamatwa na kikosi hiki na Mafwele anajua na kikosi hiki ndicho kimemkamata Soka, Mlay na Mbise”
Mbona yeye hajatekwa
 
Doh! Bado watu wanayatimba tu. Walisemaga mwendazake na sasa hayupo sijui watamsingizia nani tena.
Yeye ndiye mrithi wake...kumbuka walikuwa pamoja yeye akiwa ndiye msaidizi mkuu. Ndege wafananao huruka pamoja!
 
Yeye ndiye mrithi wake...kumbuka walikuwa pamoja yeye akiwa ndiye msaidizi mkuu. Ndege wafananao huruka pamoja!
Ni kweli ndio maana nasema walikua wanamsingizia ila mambo yao waliyafanya kwa pamoja. LAKINI KWA SABABU NI MAMBO MABAYA ALIPOTANGULIA MWENZAO WAANZA KUJITENGA NA MATENDO MABAYA WALIOFANYA PAMOJA.
 
Kuna watu walikunywa wine na konyagi kushangilia kifo cha rais Magufuli na kusema sasa nchi itatulia sababu kaipokea mama leo kiko wapi kushangilia mtu alie madarakani kwenye nchi yenye mfumo mbovu kama Tanzania ni ujinga wa mwisho sasa leo Magufuli anaishi?Ndani ya miaka miwili tayari wakosoaji wa serikali 200 washapotezwa hii sio mchezo..
 
Amesikika mheshimiwa Mbowe akimshauri mkuu wa serikali ya CCM.

1. Kwamba aunde timu ya kijaji kutafuta suluhisho la watu kupotea.

2. Kwamba awasikilize wamasai badala ya kuwashurutisha.

Kwani ni kipi wasichokijua CCM hapo?

Hawa si ndiyo wenye uthubutu wa kujiita vyura viziwi?

Atausikia vipi ushauri wa sauti kiziwi, achilia mbali chura?

Hawa si wa kushauri bali wa kukabili head on!
 
Wengi wanateteta kuwa sio Samia bali vijakazi wake ila wazungu husema 'Silence means consent', ukimya daima huchukuliwa kuwa ni ridhaa. Samia yupo kimya kuashiria ameridhia haya yote yatokee.

Kwa kila ovu linalofanyika nchini kwa sasa, ni kwa ridhaa ya Samia.
Maza mikono yake imejaa damu.
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom