Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.

Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.

Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.

Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.
Safi hiyo, Lisu naye ataenda hapo clouds jumatatu kuweka vizuri upotoshaji wowote utakaojitokeza.
 
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.

Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.

Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.

Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.
Sitashangaa kama atatangaza kujitoa katika kinyang'anyiro hiki. Mbowe ni pragmatic na atakuwa anajua kuwa hata akishinda kihalali chama chake hakitabaki salama. Nahisi washauri wake wa karibu watakuwa wamemwambia kuwa ni bora ajitoe ili akinusuru chama chake. Mtoto akililia wembe mpe.

Amandla...
 
Mbowe ni pandikizi la ccm lililo lewa madaraka kama maccm.
 
Yaani siamini kama Mwamba kachuja kama batiki la Karume 🤣🤣🤣
Aisee Shida mwamba anakuja kuharibu tena sababu sioni sehemu nyingi Lisu alishampiga pini.

Hatujui anakuja kuongea na waandishi wa habari kama Mfanyabiashara mbowe au Mwekekiti wa chadema.
 
Akatangaze kujitoa kugombea uenyekiti na kumuunga mkono Mh. Lissu ili kukinusuru chama. Chama kimegawanyika vibaya mno
Anaweza kufanya hivyo. Lakini akisema anamuunga mkono Lissu ataonekana mnafik. Ajitoe, uchaguzi, aendelee na maisha yake.

Honeymoon haichukui muda kuisha.

Amandla...
 
Kambi ya chechemela haitalala, waganga watapigiwa simu wakatege madawa kwenye mageti ya Clouds
Mbowe sasa hapati usingizi kwani hakuwa kazoea joto la uchaguzi wa ndani , alizoea kupita bila kupingwa
 
Mbowe ni pandikizi la ccm lililo lewa madaraka kama maccm
 
Mkuu kwa jinsi ulivyompamba Mbowe halaf akatangaza kujitoa katika kinyang'anyiro ili Lisu apite kwenye uchaguzi wa chama, sijui utaificha wapi sura yako!
Chawa wa mbowe wamekula pesa za mbowe wamelewa wamejitoa fahamu zote wapo busy kumtetea Mbowe hovyo bila kujali chochote na hawajui kuwa wanaendelea kumshusha mbowe zaidi
 
TAL hawezi kusimamia chama kwa miaka mitano,.
Chadema itakuwa yatima soon
 
Back
Top Bottom