Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

HUYU Jamaa ana uwezo wote wa kuwa mwenyekiti kwa Sifa za uongozi alizo nazo
 
TAL hawezi kusimamia chama kwa miaka mitano,.
Chadema itakuwa yatima soon
ishu ni kwamba hata akiendelea kuwa mwenyekiti chadema haitakuwa kama ilivyo hivi sasa, itabakiwa na wenye maslahi binafsi tu. Lile vibe halitakuwepo tena, chadema ita collapse totally chini ya mbowe again. Amechokwa hana jipya
 
Mjumbe napenda kujua sera za Mbowe ni zipi mpaka sasa. Naomba samari
Nadhani tusikilize atakayoongea kesho labda anazo sera zake zingine nje ya Katiba ya Chadema, lakini kumbuka kwamba sera zote za Chadema ziko ndani ya Katiba yake na miongozo yake, miongozo hii haikutungwa na mtu mmoja.

Ukitaka kuleta jambo jipya ni lazima uombe kwa Kamati kuu kubadili Katiba na useme kwanini
 
Hizi ni virigu tiunna pressure to ccm
Hamuna kitu uapo
 
Heshima na busara kwa baba angu mbowe nakuomba ujiuzuru TU siasa zimebadilika usiharibu heshima ulivyo jijengea muachie lisu tupambane na maccm kiulalo ulalo siasa za maridhiano kwa sasa hazitakiwa ni chuma kwa chuma TU tunahitaji mtu jasili wa kutuongoza pindi pale TU tunapo ona chama tawala kinazurimu mambo ya msingi
 
Mkuu umezunguka sana. Maana yake mpaka sasa Mbowe hana sera yeyote
 
Mjumbe napenda kujua sera za Mbowe ni zipi mpaka sasa. Naomba samari
Mkuu niliiweka huku jana, sema nini Team FAM ni Low battery na wapo tayari kudharirika ili mradi wasifie tu. 🤣🤣🤣

Maisha na dunia ya leo mtu unakuwa muoga na mnafiki ili kumpendeza mtu. Hiyo kwangu ni ngumu sana


Muangalie Lema hapo
 
Mkuu umezunguka sana. Maana yake mpaka sasa Mbowe hana sera yeyote
Sasa huu ni muda wenu wa kunadi sera za mnaowaunga mkono na kumwangusha, ni nafasi nzuri ya kushawishi wapiga kura kwamba Jamanii eeee!! Mbowe hana sera mchagueni huyu mtu wetu sera zake hizi hapa.

Msipoteze muda siku zinaisha
 
Mnahubiri demokrasia lakin m/kiti wenu kakalia kiti miaka ishirini na hataki kuachia iko wapi demokrasia mnaoihubir
 
Sasa hapo Clouds PB asubuhi watangazaji ni kina nani? Masoud Kipanya awepo na amuulize maswali, masoud amechora michoro kuhusu chadema, kuna ngumi badala ya ile alama yao ya vidole viwili, kuna makaburi mawili, itapendeza zaidi kama atamhoji mbowe kuhusu hii chadema kuelekea uchaguzi wao. Halafu mbowe mbona anaenda kufanya mahojiano kwenye media ndogo kama hiyo, si bora angeenda TBC?
 
Anajiuzulu lini uenyekiti ili apige kampeni?
Lissu hashikiki kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…