Amani iwe nanyi wana JF,
kumekuwa na desturi "mbaya" ya baadhi ya wana JF kuzungumzia mambo ya chumbani ya wanasiasa! Ndoa za Mbowe, Kikwete, Sugu, n.k. zimekuwa ndiyo case study
Kilichonifanya niandike uzi huu ni jinsi kada wa CCM aliyekuwa ofisini kwangu huku akisema kuhusu "uchepukaji" wa KUB F. A. Mbowe!!
Nilimuuliza kuhusu ndoa yake, akashindwa!
Nilimwambia anitajie
1. Mke/wake wa Kinana ni nani?
2. Watoto wa Kinana ni akina nani?
3. Mrithi wa mabilioni ya Kinana kama makampuni ni nani?
4. Nini mchango wa familia ya Kinana katika siasa?
Ndoa si siasa hata kidogo, hakuna mjanja kwenye ndoa! La sivyo watu wasingekunywa supu ya pweza iliyo na shombo!
Wapo akina marehemu
TataMadiba walishindwa kusamehe mpaka kuoa uzeeni! Ndoa ya Nyerere ilitetereka pia. Ndoa ya Bill Clinton ilitetereshwa na Monica Lewinsky
Hawa watu wanaoleta siasa kwenye ndoa hawafai hapa na labda ni watoto wadogo na hawajaoa!
Mbowe na mkewe wamesameheana na kuamua "yaliyopita si ndwele" na wamefungua ukurasa mpya