Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

Maccm yanataka kutwambia kuwa Ngorongoro siyo sehemu salama au ni kisiwa kisicho hitaji mtanzania kutembelea?

Yaani mwarabu aruhusiwe kufika kwa uhuru lkn mtanzania wa Ikungi apigwe stop ?
Yaani unawakwe zako usiende lakini Mwarabu anaingia muda anaotaka
 
Mnajua Hamjui sasa [emoji23][emoji23][emoji91][emoji209]
Utatangulia kufa wewe na utakufa umesimama kui wewe
JamiiForums-2082348249.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe aachane na haya maridhiano ya kijinga ajikite kwenye kupambana na huu utawala dhalimu
Halafu ale wapi. Kwani nje ya siasa mbowe anaajirika? Kwa elimu Gani! Hali kadhalika sugu na lema. Afadhari kidogo Lissu amesoma sheria na nje ya siasa anweza qjiliwa nakampuni yoyote ya kumlipa laki tatu kwa mwezi.
 
Mjinga wewe unadhani kila mtu hana akili kama mumeo
 
Tazama jinsi wamasaai wakifanya maombi mara baada ya mh Lissu kukamatwa leo pale karatu
 
View attachment 2744983

Tunalaani ukamataji, unyanyasaji, usumbufu unaofanywa na Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Mhe Tundu Lissu, viongozi wengine waandamizi wa ngazi mbalimbali, wanachama na wapenzi wetu huko Mkoani Arusha.

Kwa uzito huo huo, tunalaani uzuiaji wa mikutano yetu na shughuli halali za kisiasa huko Ngorongoro, Loliondo na Karatu.

Tuna hofu kubwa ya usalama wa watu wetu na ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia. Tunafuatilia kwa karibu na tunadai kuachiliwa haraka na bila masharti kwa watu wetu wote!

Freeman Mbowe
Mtandao wa X

Pia soma: Breaking News: - Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu

Maneno kuntu kutoka Kwa kamanda Mbowe.

Amri nyingine kuyaitisha matawi kuanza kukusanyika kwa majadiliano na maandalizi ya kupelekea madai rasmi ya kuachiwa Mh. Lissu na wengine ingependeza zaidi.
 
Kwa hiyo Mbowe alidhania kuachiwa kufanya mikutano ya hadhara ni ndiyo ruhusa ya kuvunja sheria??
Uwache tu huo utawala wa mabavu uendelee kuliko huu ujinga anaoendekeza Lisssu. Umeambiwa na Polisi hakuna kwenda Ngorongoro, unakaidi. Unategemea Polisi wacheke na nyani?
Sheria ipi iliyovunjwa? Au kwenda Ngorongoro mpaka upate Visa kama mgeni?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Halafu ale wapi. Kwani nje ya siasa mbowe anaajirika? Kwa elimu Gani! Hali kadhalika sugu na lema. Afadhari kidogo Lissu amesoma sheria na nje ya siasa anweza qjiliwa nakampuni yoyote ya kumlipa laki tatu kwa mwezi.
Na wewe usiwe mjinga

Mbowe kafanya Kazi Benki kuu ya Tanzania kabla ya akina Vicky na Mwigulu Nchemba

Usidhani kila mtu Elimu yake inaonyeshwa kwenye Makaratasi kama Yako 😂😂😂
 
Jamani sikilizeni Mwanahabari Digital kuna habari za kutisha.

Ingia You Tube sasa hivi.

Kuna malori na Matrekta yaliokuwa na Wanavijiji waliokuwa wanakuja kwenye mkutano wa leo Karatu.

Wamasai wameamua kuja kwa miguu hadi Karatu habari zinasema Polisi wameweka vifusi kwenye Barabara za kuingia Karatu.
 
Na wewe usiwe mjinga

Mbowe kafanya Kazi Benki kuu ya Tanzania kabla ya akina Vicky na Mwigulu Nchemba

Usidhani kila mtu Elimu yake inaonyeshwa kwenye Makaratasi kama Yako 😂😂😂
Mbowe afanye kazi bank kuu? You must be kidding. Kwa elimu Gani aliyonayo
 
Back
Top Bottom