KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
MBOWE SASA NI WAKATI WA KUPUMZIKA KWA HESHIMA CHAMA MUACHIE TUNDU LISSU.
Ikiwa Chadema itaendelea kuwa chini ya uongozi wa Mbowe basi wana miaka michache sana kwenye siasa za Nchi hii kama chama kilichodhaniwa mbadala wa CCM.
Siasa za Mbowe za kuonewa huruma kila mara Wananchi tumezichoka na kwa kweli hazina tija kwa chama chake wala kwa Watanzania maana tunataka chama kinachoweza kujisimamia chenyewe.
Mbowe mchango wake kwenye maendeleo ya demokrasia na utawala bora hapa Nchini hakuna asiyeujua wala hakuna atakayepinga namna alivyokiwezesha chama chake kufikia kilele cha siasa za ushindani Nchini cha muhimu sasa apumzike ili kulinda haya yote aliyoyapambania kwa miaka mingi.
Kwa siasa zetu sasa Chadema inahitaji Mwenyekiti wa kariba ya Tundu A. M. Lissu na wenye mwelekeo huo ili kuihuisha Chadema iweze kuendelea kuwa mbadala wa CCM vinginevyo nawaona wakielekea walipo NCCR, CUF na UDP.
Kiukweli kabisa kabisa mimi kama mtalaamu wa Sayansi ya Siasa naona Mbowe amefika mwisho hana jipya na hana namna yeyote ya kusogeza chama chake mbele kwa kifupi ameishiwa silaha na Kiongozi ukifikia hatua hii pisha wenye mawazo mapya, maono mapya, ari mpya na nguvu mpya ili chama chenu kiendelee kusonga mbele na kuwa tumaini la Watanzania wapenda mabadiliko.
Kama Political scientist nachoweza kuwashauri Chadema bure kabisa ni Mbowe kupumzika ili kuhuisha Chadema chake na harakati za kupigania demokrasia na utawala bora Nchini.
Mwenekhelonga Fadhili Sanga.