PreGE2025 Freeman Mbowe: Niseme nini? Tukiongea watasema tunawashwawashwa, wasemao ni wenye mamlaka!

PreGE2025 Freeman Mbowe: Niseme nini? Tukiongea watasema tunawashwawashwa, wasemao ni wenye mamlaka!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbowe hakulala nyumbani usiku wa kuamkia maandamano kwa sababu alijua ndio tactic wanayotumia kila wakati. Walipozingira nyumba yake walikuta hayupo.
Lissu akijua thika kuwa nyumba yake itazingirwa alilala nyumbani.
Mnyika akakimbilia kwa masista.
Lema akaja kwa ndege.
Heche hata haijulikani alikuwa wapi.
Wakina Hilda wakajikalia mbali na eneo la kukusanyika.
Mbowe akajitokeza pamoja na binti yake ambae wapambe walidai aje na watoto wake kwanza badala ya kuwachuuza watoto wa walala hoi.
Hapo nani alikuwa msanii?

Amandla...
huo usanii hukuuona uliofanyika siku ile!?
 

Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025, akisema wanaotakiwa kusema kwa sasa ni viongozi waliokabidhiwa mamlaka na chama.

Katika uchaguzi huo, Tundu Lissu alishinda nafasi ya uenyekiti kwa kupata asilimia 51.5 dhidi ya Mbowe (asilimia 48.3), huku John Heche akishinda nafasi ya makamu mwenyekiti dhidi ya Ezekia Wenje.

Soma pia: Ukimya wa Mbowe

Tangu wakati huo, Mbowe aliyetangaza kuwa atajikita kwenye biashara zake, amekuwa kimya, licha ya misukosuko iliyoibuka ikiwamo ya kuibuka kundi la G55 lenye makada wengi waliomuunga mkono, ambao sasa baadhgi yao wametangaza kukihama chama hicho.

Soma pia: Wataka Mbowe ajitokeze

Alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, Mbowe alisema: “Niseme nini? Wasemao ni wenye mamlaka.. wasije wakadai "tunawashwawashwa.”

Kauli ya Mbowe imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu Boniyai, kutangaza kwamba hakihami chama hicho na kuwaonya baadhi ya makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe.
Nirifikiri Chadema, ni project bigger than anyone life, kumbe daaa, watu wanaangslia vipnde therathini vya pesa, ambao, wakisema wataambiwa wanawaahwa ni ccm, huko ccm ndio kuna hizo mbanga!
Mfano ingetokea, huyu jamaa, na familia yake wa kaenda kumuona lisu, huko jera, na wakatoa tamko Inge kuwa Bora Sana kwa chadema,
 
Alishindwa uchaguzi kihalali, na wengi bado wanamheshimu ndani ya chama, ashirikiane na chama sasa sio kukaa kimya
Hivi kwann msiseme uongozi ushirukiane na yeye? Babala ya kumlaumu yeye peke yaķe. Navyo jua mm ushirikiano una tegemea mazingira.
 
Back
Top Bottom