Comrade Makonda hakuongea kwa bahati mbaya wala kukurupuka, aliongea ukweli mtupu. Freeman Mbowe, Ntobi, Salim Mwalimu, na Bonifas Mwita ni baadhi tu, ya watoa taarifa ndani ya Chadema. Imefika muda tuseme kila kitu kwa uwazi kwamba, Chadema ina wazalendo wachache. Wengine wote wachumia tumbo na watoa Taarifa wakiongozwa na Freeman Mbowe.
Majuzi, Mr. Mbowe akita KKKT NSHARA Machame, alitangaza hadharani kwamba, Rais Samia alitoa mchango wa TZS 150million, ambayo kwa lugha nyingine ni “Endorsement” ya Rais Samia 2025. Mbowe amewatangazia watanzania kwamba mgombea wake 2025 ni Samia Suluhu Hassan. Bila kumung’unya maneno niulize maswali mawili tuu. Zile Toyota Landcruiser Mr. Mbowe alizitoa wapi? Na ile Chopper, fedha zake zilitoka wapi?
Kadhalika, Mr. Freeman Mbowe aliwaalika Covid-19 wakiongozwa na Mr. Alima Mdee kwenye hiyo harambee ikimaanisha kwamba, kwa muda mrefu, Mr. Mbowe amekuwa akiwakumbatia COVID-19 ndani ya CDM. Jiulizeni, Tulia Ackson anatoa wapi jeuri ya kuwakumbatia hao COVID-19? Wote wanalindwa na Mr. Freeman Mbowe na hawakwenda KKKT NSHARA Machame Kimakosa. Wote walienda kueneza mema ya viongozi wa CCM kwa mualiko wa Mr. Mbowe..Kwa maana hiyo, Mr. Mbowe na Covid-19 ni kitu kimoja. Kadhalika Samia na Mbowe ni kitu kimoja. Mbowe ni mtoa taarifa
Tukiwa wana CCM. Hawa watu wa CHADEMA wanatukera. Either waingie CCM au wanyamaze. Sisi hatuwataki maana wanaonyesha kufanya siasa za makueni. wanaunga mkono siasa za makundi. Wanamuunga mkono kundi la Samia.
Mr. Freeman Aikeli Mbowe, chagua moja. Baki ndani ya CDM mazima, au njoo ccm kundi la Samia 100%. Hatupendi unalolifanya maana unawavuruga Chadema na wana CCM vilevile. Kama umeshiba asali, basi jiuzulu uenyekiti na kukaa kimya, ila sisi hatukutaki ndani ya CCM. Tunajua lengo lako, ni kutengeneza ukaribu tena na Rais Samia, maana taarifa zilikufikia za Samia kuchukia ulivyomponda majukwaani baada ya kula hela zake za kukodi Elicopter na Magari ya Mikutano mikoani.
Kwanza naandika kama Mtanzania independent ambaye sina chama, na kwa kweli nina sympathy na upinzani zaidi.
Kwa hiyo, siandiki kama chawa wa CCM.
Kwa maneno mengine, ningefurahi sana Mbowe angekuwa anafanya vizuri.
Mbowe ana ji contradict sana. Kama Mwenyekiti wa CHADEMA alitakiwa kuelewa kanuni za msingi za Separation of Church and State.
Kwa kumualika Samia na kukubali mchango wa shilingi milioni 150 kwenye shughuli ya kanisa lake kwao, inakuwa kama kakubali kuhongwa na Samia.
Mimi sikuwa na tatizo Mbowe kushiriki maongezi ya maridhiano, angeweza kusema yeye ni kiongozi moderate aliyekuwa anatafuta maridhiano tu. Ingawa hata hayo yalikuwa yanakwenda kwenye dead end, tulijua tu. Lakini, mara nyingine kiongozi wa upinzani anahitaji kuchukua njia inayompeleka kwenye dead end ili kutuonesha kuwa alikuwa na nia ya maridhiano, lakini upande wa pili umekwamisha hapa na hapa. Ndiyo maana hata mahakamani upinzani huwa unafungua kesi ambazo tunajua utashindwa, lakini wanataka kuweka rekodi kwamba tulifungua kesi hivi, mahakama ikatuonea hivi.
Kwa hiyo, hata kwenye maridhiano alikopingwa na watu wengi, mimi niliona kuwa Mbowe bado ana nafasi ya ku make sense.
Lakini huku kwenye kumualika Samia atoe shilingi milioni 150, Mbowe kajitia doa sana. Yani hata kiongozi wa CCM kumualika Samia na Samia kuchangia shilingi milioni 150 kwenye kanisa la huyo kiongozi ni tatizo. Anavunja kanuni za Separation of Church and State.
Nyerere katawala miaka 24. Alikuwa anakwenda kanisani kila siku akiwa Dar. St. Peters asubuhi kabisa utamkuta pale. Lakini hakufanya mchezo huu wa kuchangia kanisa pesa. Si kwa style na kiasi hiki.
Mbowe kama Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anatakiwa kujua kuwa, demokrasia ni pamoja na separationnof church and state.
This is such a big disappointment.
Kama huyu kiongozi mkubwa hivi CHADEMA anaweza kufanya strategic mistake kubwa hivi hadharani, huko nyuma ya pazia anaboronga vipi?
In law, there is a principle. Justice must not only be done. It must appear to be done. Democracy as part of the rule of law falls under the same principle. It must not only be fulfilled, it must appear to be fulfilled.
Appearances matter. Right now, it appears as if Mr. Mbowe has been bought. Very cheaply indeed.
Kwa uongozi huu bado CHADEMA inategemea kuishinda CCM?
Au hawa viongozi wa CHADEMA wanajua kabisa CCM hawawezi kuishinda, wameamua kugawana mazuri ya nchi tu huku wakiwapiga wananchi magirini tu?