Pre GE2025 Freeman Mbowe: Shutma za Lissu dhidi yangu ni za uongo

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Shutma za Lissu dhidi yangu ni za uongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Kwenye mahojiano na Salim Kikeke kupitia, Crown FM, Mbowe amefunguka kuwa;

"Mimi kama Mwenyekiti wa chama ni tabia yangu ni historia yangu, sijawahi kuingia kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta sifa na mimi nilikuwa mtu wa kujenga na kulea vipaji vingi kwa miaka yote, Tundu Lissu mimi nimemuingiza kwenye chama na tukamjenga na tukamsaidia kwa njia zote na yeye akakisaidia chama kwa njia mbalimbali".

"Swali la Lissu kunishambulia angelijibu vizuri yeye kwa sababu hakuna shutma hata moja anayoeleza hadharani dhidi yangu ambayo ni ya kweli, na tumeshamtaka kama una ushahidi wa chochote lete kwenye vikao vya chama." - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
IMG_2252.jpeg

Pia, Soma;

Mpambano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu: Wajue wagombea hawa wawili

Ezekia Wenje: Wapambe wanawagombanisha Mbowe na Lissu
 
Kama hauja "itaka" ungepita kimya tu! Hata, kwenye kuaga maiti, sio wote wanaopita mbele ya jeneza, wanaliangalia, wanapita huku wanaangalia pembeni!
Mbowe kayasema wapi na lini, alikuwa akiongea na Nani...

Ni rahisi Sana tu kuonyesha upeo wako wa kuanzisha mada.
 
Mbowe ameiharibu kazi aliyoifanya kwa miaka 20+ yeye mwenyewe kwa mikono yake. Kama kweli ni mkongwe ameshindwaje kuyajua mahitaji ya wanachama na wafuasi wa Chadema kuwa wanataka mabadiliko? Mbona kila mwenye mapenzi na Chadema anaona kuwa Mbowe ame overstay kwenye uenyekiti?
 
Haitwi mbowe bali anaitwa mseven wa machame
 
Back
Top Bottom