Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Porojo tu.
Hawana uthubutu, matamko yamekua mengi mnoooo
 
Hiyo siku nimeitazama kwenye calendar nimekuta ni siku ya jogging ya wanajeshi nchi mzima

Okay ngoja tusubili tuone itakiwaje
 
Sawasawa
Sasa hapa imekaa vyema,tutaingia Barabarani
Hiyo ndiyo LUGHA ambayo Watawala wanaielewa kuliko Scotland Yard.

Tunaingia Barabani Maandamano ya AMANI hizi ndio Pressure zinazotakiwa.

🫡🫡 Salute Kamanda.
 
Hawa jamaa kwakuwa wanakula bure wanadhani wote tupo hivyo sijui nani awaeleze kwamba tulio wengi kama kweli watafanikiwa tutalala na njaa. Kwani hatuna mbinu mbadala ya kufanya hao mahasimu wenu wawasikie? Nikweli hoja ipo na ni kweli kabisa kuna mambo hayaendi sawa kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji pia ukatili kila kona kuanzia kwa raia mpaka kwa waajiriwa.

Nadhani kuna namna tunaweza kufanya bila kuathiri kipato chetu au afya zetu tengenezeni utaratibu wa kufahamisha umma ili kwenye sanduku la kura tupige kwa hasira na kuzilinda ole wao wabadili matokeo hapo sasa tuitoe siku nzima kama sadaka pia wanazuoni waje na utafiti kuona namna bora ya kuifanya nchi hii iwe yenye kuweka viongozi watakao tekeleza mahitaji ya wananchi wote pia wapinzani waeleze wao tukiwachagua watafanya nini tofauti na hawa waliopo?
 
Ulikuwa wapi mwenyekiti tulikuwa tunakushangaa
 
Kama tunavyojua chama Cha waoga tanzania ni chadema ambacho Kila siku wanasema wanaandamana halafu polisi wanajua kabisa chadema ni makunguru ikitokea chadema na wafuasi wake wameandamana tarehe 23 nipigwe ban sababu sijawahi kuona Cha Cha waoga kama chadema Africa hii tena wakishaona mmoja wao kashugulikiwa hua wanafyata mkia ndio maana Leo polisi wamewaambia kabisa wakigusa ardhi ya barabara tarehe 23 ni kichapo na wataona Cha mtema kuni
 
Baada ya taarifa hii Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu,
ushauri wangu kwa CHADEMA ni ule ule Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!
P
 

Maneno haya yamejaa busara na hekima
 
Ngoja nikuulize swali Moja tu dogo, hivi mpaka lini Chadema, wataendelea kufanya huo unaouita uvumilivu Kwa madhila wanayofanyiwa??

Tujikumbushe, miaka zaidi ya 7 iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, alimiminiwa risasi za kutaka kumuua.

Hao hao Polisi wanaendelea kudai kuwa upelelezi wa tukio Hilo bado unaendelea!

Hivi upelelezi Gani unaoweza kuendelea katika tukio lililo la wazi kabisa, kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wa mfumo??

Njia pekee ya kutokemeza udhalimu huu, unaofanywa na Jeshi la Polisi, chini ya uangalizi wa karibu kabisa wa chama Cha CCM, ni kujitoa muhanga na kuandamana Kwa amani, ambapo ni halali Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu.

Vitisho wanavyovitoa Polisi, kama kawaida yao ni uvunjifu wa Katiba ya nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…