Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Kanuni ya uvumilivu ni kuvumilia mpaka mwisho, kama Chadema sasa ndio wamefika mwisho wa uvumilivu wao, haya na waandamane tuwaone!Ngoja nikuulize swali Moja tu dogo, hivi mpaka lini Chadema, wataendelea kufanya huo unaouita uvumilivu Kwa madhila wanayofanyiwa??
Ni kweli hili ni tukio baya kabisa na sote tulilaani.Tujikumbushe, miaka zaidi ya 7 iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, alimiminiwa risasi za kutaka kumuua.
Hapa ni uwezo mdogo wa polisi wetu kuchunguza,Hao hao Polisi wanaendelea kudai kuwa upelelezi wa tukio Hilo bado unaendelea!
Una uhakika?Hivi upelelezi Gani unaoweza kuendelea katika tukio lililo la wazi kabisa, kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wa mfumo??
Ni kweli maandamano ni haki ila usalama kwanza!Njia pekee ya kutokemeza udhalimu huu, unaofanywa na Jeshi la Polisi, chini ya uangalizi wa karibu kabisa wa chama Cha CCM, ni kujitoa muhanga na kuandamana Kwa amani, ambapo ni halali Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu.
Ni kweli huu ni uvunjifu wa katiba, ila pia ni katiba hiyo hiyo imeruhusu usalama kwanza, ukiona kuna hatari za kiusalama, katiba inawekwa pembeni, usalama kwanza.Vitisho wanavyovitoa Polisi, kama kawaida yao ni uvunjifu wa Katiba ya nchi yetu
P