X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,605
- 1,843
Miaka sita baada ya kuchapishwa ilani ya humanism, vita vya pili vya Duniya vikaripuka
Katika aya hii ya Quran Mwenyezi Mungu anasema, Je! Binadamu anafikiri kuwa ataachwa bure tu (asipewe amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je! Hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (kuwa mtu kamili)? Kisha akamfanya namna mbili. Mwanaume na mwanamke. Je! Hakuwa hayo ni muweza wa kuhuisha wafu?
Hapa Mwenyezi Mungu anawakumbusha binadamu kuwa wao ni viumbe vyake. Pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa bali anawajibika kwa Mwenyezi Mungu.
Dai kuwa binadamu hawakuumbwa ndio msingi wa falsafa ya humanism. Vipengele viwili vya ilani ya kwanza ya Wahumanisti vinatoa ufafanuzi wa itikadi hii.
Zaidi ya hivyo Wahumanisti wanashikilia kuwa sayansi inaunga mkono madai haya. Lakini ni waongo wakubwa.
Tokea ilani yao ya kwanza ilipochapishwa, hoja mbili ambazo wanahumanisti wamezitoa kama hakika za kisayansi, kwamba ulimwengu ni wa milele na wa kievolusheni, zote zimevunjiliwa mbali.
Dhana kwamba ulimwengu ni wa milele ulivunjiliwa mbali na mlolongo wa vumbuzi za angani zilizofanywa wakati ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipokuwa inaandikwa.
Vumbuzi kama vile ulimwengu kutanuka, chanzo cha mionzi ya angani na mahesabu ya uwiano ya Haidrojeni hadi Helium, zimethibitisha kuwa ulimwengu ulikuwa na chanzo chake na kwamba ulitokea kwa mlipuko mkubwa- Big Bang takriban miaka bilioni 15 au 17 iliyopita.
Ingawa wale wanashabikia falsafa ya kihumanisti na ya kilahidi walikataa kuikubali nadharia ya Big Bang lakini hatimaye walishindwa vibaya sana kutokana na ushahidi wa kisayansi ambao umejitokeza.
Jamii ya wanasayansi hatimaye ikaikubali nadharia ya Big Bang kwamba ulimwengu ulikuwa na chanzo chake. Hivyo, Muatheisti Anthony Flew alilazimika kukiri hivi;
.Sasa nitaanza kukiri kuwa Muatheisti lazima atatizike kwa hizi fikra za sasa za maumbile. Kwani inaonekana kuwa wanakosmolojia wanatoa ushahidi kuwa kile alichodai mtakatifu Thomas hakiwezi kuthibitishwa kifalsafa, hii ikiwa na maana kuwa ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake.
Nadharia ya evolusheni ambayo ndio hoja kuu iliyomo katika ilani ya kwanza ya humanisti, ikaanza kupoteza nguvu miongo kadhaa baada ya kuandikwa kwake.
Inafahamika hivi leo kuwa ubabaishaji uliofanywa na wanaevolusheni na Waatheisti (na bila shaka Wahumanisti) kama vile A.I. Oparin na J.B.S Haldane katika miaka ya thelasini kuhusiana na chanzo cha uhai hauna msingi wa kisayansi.
Viumbe haviwezi kutokea kwa bahati nasibu kutokana na maada isiyo na uhai kama ilivyodaiwa katika ubabaishaji huo. Kumbu kumbu ya mabaki ya kale inaonesha kuwa viumbe hai hawakuwa hivi walivyo kutokana na hatua za mabadiliko madogo madogo bali walitokea kuwa pamoja wakiwa na sifa zao mbalimbali.
Ukweli huu umekubaliwa na wanaevolusheni wenyewe tangia miaka ya sabini. Sayansi ya viumbe hivi leo imebainisha kuwa viumbe hai hawakutokana na bahati nasibu na kanuni za maumbile bali katika kila kiumbe kuna mfumo madhubuti unaothibitisha kuwa msaniii mwenye hekima ndiye aliyeviumba. Kwa maelezo zaidi rejea kitabu kiitwacho Darwinism refuted. Zaidi ya hivyo, lile dai la uongo kuwa imani ya dini ndiyo sababu inayokwaza watu kuendelea na kuwatumbukiza matatizoni limetupiliwa mbali na ushahidi wa kihistoria. Wahumanisti wamedai kuwa kuondolewa kwa imani ya dini kutawaletea watu faraja na furaha, lakini hali ya mambo imekuwa kinyume chake.
. Vita hii ni kielelezo cha kihistoria cha misiba mikubwa iliyoletwa na itikadi za kifashisti za kisekula. Ikachipuka itikadi ya kikomunisti ya wahumanisti kwanza ilianzia kwa watu wa Urusi, kisha kwa watu wa China, Cambodia, Vietnam, Korea kaskazini, Cuba na katika baadhi ya nchi za Afrika na Latin Amerika. Ulifanyika ushenzi usio na mfano. Jumla ya watu milioni 120 waliuliwa na tawala au Jumuiya za kikomunisti. Ni dhahiri kuwa kundi la Wahumanisti wa magharibi (mabepari) nalo limeshindwa kuleta amani na furaha katika jamii zao na katika maeneo mengine ya Duniya. Kuvunjwa kwa hoja ya Wahumanisti juu ya dini pia kunadhihirika katika fani ya saikolojia. Misingi ya dhana ya Kiatheisti ilibatilishwa na matokeo ya tafiti tokea mwanzoni mwa karne ya ishirini (The Freudian myth). Patric Glynn wa chuo kikuu cha George Washington anaufafanua ukweli huu katika kitabu chake kiitwacho God, The Evidence, The Reconciliation of Faith and reason in a Post Secular World.