Dhana ya ‘humanism'
Yasadikiwa na wengi kuwa Humanism ndio itikadi madhubuti. Inampandikiza mtu hisia za upendo, utulivu na Udugu. Lakini kifalsafa dhana hii ina maana kubwa zaidi. Humanism ni utaratibu wa fikra ambao unaichukulia dhana ya ubinadamu kama ndio msingi na lengo lake kuu. Kwa maneno mengine inawataka watu wajitenge mbali na Mungu, Muumba wao na washughulike na maisha yao na utu wao. Kamusi ya Kiingereza iitwayo Common dictionary inaliainisha neno humanism kama ni mfumo wa itikadi uliojengwa juu ya msingi wa maadili, sifa na tabia ambazo zinaaminika kuwa bora zaidi kwa vigezo vya binadamu wenyewe bila kutegemea muongozo wowote wa Kiungu.
Ainisho la wazi zaidi la humanism limetolewa na wale wanaounga mkono itikadi hii. Mmoja kati ya wapiga debe wakuu wa dhana ya humanism ni bwana Corliss Lamont. Katika kitabu chake kiitwacho The philosophy of Humanism, mwandishi huyu ameandika hivi: Kwa ujumla Humanism inaamini kuwa maumbile yanatokana na mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo msingi wake ni nguvu ya maada. Maada ndio msingi wa Ulimwengu na kwamba nguvu za Kiungu hazipo. Dhana ya nguvu za Kiungu, kwa upeo wa binadamu, haina uthibisho. Kwamba watu hawana roho za kudumu milele yaani zisizo kufa na ulimwengu kwa ujumla hauna Mungu aliyeuumba wala Mungu wa milele.
Kama tunavyojionea wenyewe katika nukuu hizo, itikadi ya humanism karibu inafanana kabisa na Itikadi ya atheism, na ukweli huu unakubaliwa bila ubishi na wanahumanisti. Kulikuwa na ilani mbili muhimu zilizochapishwa na wanahumanisti katika karne iliyopita. Ilani ya kwanza ilichapishwa mwaka 1933, na ikapitishwa na watu muhimu wa wakati huo. Miaka arobaini baadaye, mnamo mwaka 1973, ilani ya pili ya wanahumanisti ilichapishwa. Ilani hii iliithibitisha ile ya kwanza lakini ikatiwa nyongeza kufuatia hatua fulani za maendeleo ambazo zilipigwa wakati huo. Maelfu ya wanafikra, Wanasayansi, Waandishi na Wanahabari walisaini ilani ya pili ambayo inaungwa mkono na chama cha harakati za wana humanisti wa Amerika.
Tunapoziangalia ilani hizi, tunakuta kuwa katika kila ilani kuna huu msingi mmoja mkuu, ambao ni Dhana ya atheism ambayo inasema ulimwengu na wanadamu hawakuumbwa bali wanaishi kwa kujiendesha wenyewe, kwamba binadamu hawawajibiki kwa mamlaka yoyote isipokuwa kwao wenyewe, na kwamba Imani juu ya Mungu imedumaza maendeleo ya watu na jamii. Kwa mfano vipengele sita vya kwanza vya ilani ya kwanza vya wanahumanist ni hivi vifuatavyo:
Mosi: Wanahumanist wanaitakidi kuwa ulimwengu unajiendeshea wenyewe maisha yake na haukuumbwa.
Pili: Dhana ya humanism ina itakidi kuwa Mtu ni sehemu ya maumbile na kwamba ameibuka kutokana na mfumo unaojiendesha wenyewe.
Tatu: wakishikilia mtazamo wa maisha wakioganiki, Wanahumanisti wanaona kuwa dhana ya pande mbili za nafsi na mwili lazima ipingwe kabisa.
Nne:Itikadi ya humanism inatambua kuwa utamaduni wa kidini wa mtu na ustaarabu wake kama ulivyoelezwa na historia ni zao la hatua za polepole za maendeleo zitokanazo na mahusiano baina yake na mazingira yake na urathi wa jamii yake. Mtu anayezaliwa katika utamaduni fulani kwa kiasi kikubwa anajengeka kwa utamaduni huo.
Tano: Dhana ya humanism inatangaza kuwa maumbile ya ulimwengu yalioelezwa na sayansi ya leo yanatupilia mbali nguvu yoyote ya mbinguni kuhusiana na maadili ya binadamu.
Sita: Tunaamini kuwa dhana za theism, deism, modernism na aina kadhaa za itikadi mpya zimepitwa na wakati.
Katika vipengele hivyo tunaiona wazi nafasi ya falsafa ya common ambayo inajidhihirisha yenyewe kwa majina ya materialism, Darwinism, atheism na agnosticism. Katika kipengele cha kwanza dhana ya ulahidi ya uhai wa milele wa ulimwengu imewekwa wazi.
Kipengele cha pili kinasema kuwa binadamu hawakuumbwa, hivi ndivyo inavyosema nadharia ya evolusheni. Kipengele cha tatu kinakanusha kuwepo kwa roho kikidai kuwa viumbe wanatokana na maada. Kipengele cha nne kinapendekeza mageuzi ya kiutamaduni na kinakanusha kuwepo kwa silika aliyopewa bindamu (Silika maalum ya binadamu katika maumbile).
Kipengele cha tano kinakanusha mamlaka ya Mungu juu ya ulimwengu na walimwengu na kipengele cha sita kinakataa Imani juu ya Mungu. Itakumbukwa kuwa madai haya ndiyo yale yale ya zile duru zenye chuki na dini sahihi. Sababu ni kuwa dhana ya humanism ndio msingi mkuu wa hisia zote zinazopinga dini. Hii ni kwa sababu dhana hii inasema kuwa mtu ataachwa hivyo hivyo bila kuhesabiwa. katika historia yote. Huu ndio umekuwa msingi wa madai ya kumkanusha Mungu. Katika aya moja ya Qur'an Mwenyezi Mungu anasema:
Je! Anafikiri binadamu kuwa ataachwa bure, (asipewe amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je! Hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (kuwa mwanadamu kamili)? Kisha akamfanya namna mbili, Mwanaume na Mwanamke. Je ! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?
Mwenyezi Mungu anasema watu hawakuachwa tu hivi hivi na anawakumbusha kuwa wao ni viumbe vyake. Hii ni kwa sababu pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu, basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa bali anawajibika kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa sababu hii, dai kuwa binadamu hawakuumbwa ndio limekuwa msingi wa falsafa ya humanism Vipengele viwili vya ilani ya kwanza ya wanahumanisti vinatoa maelezo ya itikadi hii. Isitoshe wana humanisti wanashikilia kuwa Sayansi inaunga mkono madai haya. Lakini ni waongo. Tokeya ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipochapishwa Premesia mbili ambazo wanahumanisti wameziainisha kama hakika za kisayansi, kwamba ile dhana kuwa ulimwengu ni wa milele pamoja na nadharia ya evolusheni zote zimesambaratika.
1. Dhana kuwa Ulimwengu ni wa milele ilivunjiliwa mbali na mlolongo wa vumbuzi za angani zilizofanywa pale ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipokuwa inaandikwa.. Vumbuzi kama vile ulimwengu kutanuka, chanzo cha mionzi ya angani na mahesabu ya uwiano ya Haidrogen hadi helium, zimeonyesha kuwa ulimwengu ulikuwa na chanzo chake na kwamba uliibuka kutokana na hamna takribani miaka bilioni 15-17 iliyopita kwa mlipuko mkubwa ulioitwa Big Bang.
Ingawaje wale wanaounga mkono falsafa ya kihumanisti na kilahidi walikataa kukubali nadharia ya Big Bang lakini hatimaye walishindwa kabisa. Kutokana na ushahidi wa kisayansi ambao umejitokeza, jamii ya wanasayansi hatimaye imeikubali nadharia ya Big Bang kwamba ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake na hivyo wanahumanisti hawana hoja. Hivyo mwanaatheist Antony Flew alilazimika kukiri hivi:
.Sasa nitaanza kukiri kuwa mwanaatheisti lazima atatizike kwa hizi fikra za sasa za maumbile. Kwani inaonekana kuwa Wanakosmolojia wanatoa ushahidi kuwa kile alichodai Mtakatifu Tomas hakiwezi kuthibitishwa kifalsafa hii ikiwa na maana kuwa ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake.
2. Nadharia ya evolusheni ambayo ndiyo hoja kuu iliyomo katika ilani ya kwanza ya humanism ikaanza kupoteza nguvu miongo kadhaa baada ya kuandikwa kwake. Inafahamika hivi leo ubabaishaji uliofanywa na wana evolusheni na wakiatheisti (na bila shaka wakihumanisti), kama vile A.I. Oparin na J.B.S. Haldane katika miaka ya thelathini kuhusiana na chanzo cha uhai hauna msingi wa kisayansi.
3. Viumbe haviwezi kutokea kwa bahati nasibu kutokana na maada isiyo na uhai kama ilivyodaiwa katika ubabaishaji huu. Kumbukumbu ya mabaki ya kale inaonyesha kuwa viumbe hai hawakuwa hivi walivyo kutokana na hatua za mabadiliko madogo madogo bali walitokea kwa pamoja wakiwa na sifa zao mbali mbali.
4. Ukweli huu umekubaliwa na wana evolusheni wenyewe tangia miaka ya Sabini. Sayansi ya viumbe hivi leo imebainisha kuwa viumbe hai hawakutokana na bahati nasibu na kanuni za maumbile bali katika kila kiumbe kuna mfumo madhubuti unaothibitisha kuwa Msanii mwenye hekima ndiye aliyeviumba. Ukitaka maelezo zaidi rejea kitabu kiitwacho, Darwinism Refuted.
Zaidi ya hivyo dai la uongo kuwa imani ya dini ndio sababu inayowakwaza watu kuendelea na kuwatumbukiza katika mifarakano limetupiliwa mbali na ushahidi wa kihistoria. Wanahumanisti wamedai kuwa kuondolewa kwa imani ya dini kutawaletea watu furaha na faraja. Hata hivyo hali imekuwa kinyume cha mambo.
Miaka sita baada ya kuchapishwa kwa ilani ya humanism, vita vya pili vya Duniya vikalipuka, hii ni kumbukumbu ya misiba mikubwa iliyoletwa na itikadi za kifashisti za kisekula. Itikadi ya Humanism ya Ukomunisti ikachipuka, kwanza ilianzia kwa watu wa Urusi kisha kwa watu wa China, Cambodia, Vietnam, Korea kaskazini, Cuba na katika baadhi ya nchi za afrika na Latin Amerika, kulikuwa ni ushenzi usio na mfano.
Jumla ya watu Milioni 120 waliuawa na tawala za Kikomunisti au jumuiya za kikomonisti. Ni dhahiri kuwa kundi la wanahumanisti wa Magharibi (mifumo ya kibepari) nalo limeshindwa kuleta amani na furaha katika jamii zao na katika maeneo mengine ya Duniya.
Kuvunjwa kwa hoja ya humanism juu ya dini pia kumedhirishwa katika fani ya saikolojia. The Freudian myth, msingi wa dhana ya kiatheist tokea mwanzoni mwa karneya ishirini imebatilishwa na matokeo ya uchunguzi. Patric Glynn wa Chuo Kikuu cha George Washington anaufafanua ukweli huu katika kitabu chake kinachoitwa
God: The Evidence, The Reconciliation of Faith and Reason in a PostSecular World.