Imani kali ya ukatoliki ndio ilimzuia mwalimu kuingia katika freemason lakini kuna wakati ilikuwa karibu kuingia kutokana na mashinikizo mbalimbali ya marafiki zake kama kina Chifu Fundikira, George Kahama na wengineo. Kwa Tanzania mwanzoni llikuwa kundi la Wazungu na wahindi tu lakini baadae wakajiunga kina sisi na kimantiki ni kuwa kundi hili lilitambulika kuwa muhimu katika kurahisisha mafanikio kibiashara na kisiasa.
Kuhusu Ben hakuna ubishi ni mmoja wao na ndiye alikuwa chaguo lao hata miaka mitatu kabla ya uchaguzi wa 2005. Wapo wengi tu lakini kutokana na ukame wa information miongoni mwa watanza tunaishia kuwaita dini ya mashetani.
Ni kweli kuwa kwa nje freemason inapswa kuwa kundi la watu waliojitolea kutumia elimu, vipaji na uwezo wao kisiasa, kiuchumi na kijamii kusaidia jamii zao na dunia kwa ujumla. Lakini kama ilivyo makundi mwengine mengi yanayoendeshwa kwa usiri, Freemasonry imekuwa kundi la kulinda, kuunganisha na kuendeleza ufisadi. Lakini hali hii inatofautiana kutoka chapter/lodge moja haid nyingine..
Makundi mengine yanayoshabihiana na hili na mara nyingi huwa ni front ya freemasonry ni Rotary Clubs, Lion Clubs na hata rotaract ambayo mara nyingi huwa ni recruitment ground for young members.
Kitabu cha Andy Chande ni muhimu kukisoma ingawa kuna mengi yalilazimishwa kuondolewa kwa maslahi ya kundi hilo, serikali kadhaa na wanasisa na watu binafsi.
Tanzanianjema