roman empire ilipoanguka tu ,kilichoibuka ni roman catholic ,hii inathibitishwa hata na biblia
Nabii Danieli anaiona PEMBE NDOGO inazuka ghafla ambayo iko kwa namna hii,
"..... na tazama, katika pembe hiyo MLIKUWA NA MACHO KAMA MACHO YA MWANADAMU, na KINYWA KILICHOKUWA KIKINENA MANENO MAKUU"- (Dan.7:8)
-Pembe Ndogo inaonekana ina macho kama ya mwanadamu, na mbaya zaidi Pembe Ndogo INANENA MANENO MAKUU. Hapa tunakuja kumwona Nabii Yohana akija kuzungumzia juu ya Pembe Ndogo aliyoiona Nabii mwenzake Danieli, lakini Yohana katika njozi yake alimwona Mnyama akitokea Baharini- (Ufu.13:1). Mnyama toka Baharini ndiyo yuleyule anayezungumziwa na Nabii Danieli kama Pembe Ndogo. Sasa, tabia ya Mnyama toka Baharini naye ANANENA MANENO MAKUU tena YA MAKUFURU. Nabii Yohana alisema,
"Naye akapewa kinywa cha kunena MANENO MAKUU, YA MAKUFURU"- (Ufu.13:5)
-Naam, baada ya Utawala wa Rumi ya Kipagani, kilichofuata ni Utawala wa Rumi ya Kidini, yaani Upapa(Sio Papa, bali ni Upapa), hivyo Pembe Ndogo au Mnyama toka Baharini ni Upapa ambao umetokea kwenye ufalme wa Rumi ya Kipagani na ndo maana analiongoza kanisa la Roma(Roman Catholic Church), yaani katika Ufalme wa Roma, kuna kanisa ambalo linaongozwa na Pembe Ndogo. Lakini, tunaona Pembe Ndogo inanena MANENO MAKUU YA MAKUFURU. Je, KUFURU NI KITU GANI? Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Uk.278 inasema,
"Kufuru ni sema jambo ambalo ni kinyume na imani ya dini "
-Kumbe, Kufuru ni lazima ihusiane na imani. Hakuna kufuru katika uchumi, siasa, n.k., bali kufuru imejikita katika imani au dini. Kwa ufupi ni kuwa KUFURU NI KUSEMA KINYUME NA MUNGU. Hii ni kulingana na muktadha wa Biblia. Ndo maana Nabii Danieli akiwa anaielezea Pembe Ndogo, alisema,
"Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu,.......; naye ataazimu kubadili majira na sheria...."- (Dan.7:25)
“Kwa kutumia mbinu hii ya kutafsiri unabii, kanisa la Roma lilionekana wazi kuhusika
na unabii huu wa pembe ndogo katika Daniel 7, na mnyama wa Ufunuo 13:1, mwanamke
wa Ufunuo 17, ikiwa ni pamoja na kichwa cha kanisa kuwakilisha Mtu wa Kuasi wa 2
Wathesalonike 2. Kadri mafundisho haya yalivyozidi, kanisa la Roma lililazimika
kujilinda dhidi ya kuongezeka kwa ushahidi wa unabii wa Biblia kulihusisha kanisa hilo.
Hivyo upapa ukaanza kuweka mipango ya kuwapinga waprotestant kwa kuanzisha
‘Jesuit society’ ili kisaidie kufundisha mafundisho ya kanisa na kuharibu mafundisho na
vitabu vyote vilivyokuwa kinyume na kanisa na kuanzisha “Holy Office of the
Inquisition” maalumu