'Friends of Raila'...(F.O.R.A.) watangaza kuwa bosi wao ameshinda kura za jumla nchi nzima

jamani, Uhuru kenyatta ameshinda huu uchaguzi, kama odinga akileta za kuleta, kwakweli hatutamuelewa. mimi mwenyewe nilikuwa supporter wa odinga, lakini kutokana na kura zilivyotoka, asiyekubali kushindwa si mshindani. pamoja na yote, tuseme ule ukweli tu, Wakenya hawako fair sana, waache ukabila, wakikuyu waache ukabila, wametawala mno, wamekula mno hiyo nchi tangu babayake uhuru awe raisi, wamejilimbikizia sana mali ardhi n.k, ilikuwa fair kama wakiwaachia na wajaluo au watu wengine wawe maraisi wa hiyo nchi hapo ndo ukabila ungekuja kuisha, lakini kwa trend hii ya sasa, hakika ukabila kenya hautakuja kuisha kwasababu kama uhuru akishinda, chuki dhidi ya wakikuyu itakuwa juu kuliko ilivyokuwa mwaka 2007/2008. waache ukabila, wakikuyu acheni ukabila, muone aibu sasa wakati mwingine.

mkuu zimetangazwa kura milioni 5.7 kati ya milioni 10 mbona bado sana!
 
Mpaka sasa 14:51 Kenyatta 2,590,393 (53.87%) wakati Odinga 2,001,651 ( 41.59%) ninachokiona hapa ni ODIGA kudondoka kifo cha mende. Jibabu Odinga hiloooooooooo waachie vijana kina Uhuru Kenyatta waendeshe nchi we kavua samaki
 
Mkuu hayo ni mawazo yangu binafsi wala hayawakilishi mawazo ya aliyenituma hapa. Naomba Nieleweke hivyo!!! Frankly speaking kura bado zinahesabiwa halafu watu wanakuja na vitisho vya kusema wao wana tallying centre yao inayoonyesha kwamba mtu wao anafanya vizuri. Huu ni upuuzi na kutafuta kuja kuleta machafuko endapo at the end of the day Raila hatatangazwa mshindi!!!

Tiba
Aksante kwa ufafanuzi huo mkuu Tiba.
Ukiangalia kwa undani hakuna ubishi kwenye Total vote Kenyatta atashinda,shaka yangu ni kuweza kufikia kigezo cha pili cha kupata 24 county out of 47 kwani yeye anashinda sehemu yenye high registered voters kama Rift Valley na Central.
 
Mpaka sasa 14:51 Kenyatta 2,590,393 (53.87%) wakati Odinga 2,001,651 ( 41.59%) ninachokiona hapa ni ODIGA kudondoka kifo cha mende. Jibabu Odinga hiloooooooooo waachie vijana kina Uhuru Kenyatta waendeshe nchi we kavua samaki

For sure I hate this comment. Unaonekana hujakomaa hata kidogo. Je wewe ni mwimba taarabu? what are you doing here eh. Sio swala la uzee na ujana nya****mb***f
 
Aksante kwa ufafanuzi huo mkuu Tiba.
Ukiangalia kwa undani hakuna ubishi kwenye Total vote Kenyatta atashinda,shaka yangu ni kuweza kufikia kigezo cha pili cha kupata 24 county out of 47 kwani yeye anashinda sehemu yenye high registered voters kama Rift Valley na Central.

Ndugu yangu hicho bado ni kitendawili ambacho sijajua kama kitateguliwa kwa urahisi. Tusubiri tuone mambo yatakuwaje ingawaje kwa matokeo ya hivi karibuni, Raila ameanza kupanda wakati Uhuru anashuka. Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, kupanda kwa Raila kunaweza tu kumzuia Uhuru asipite moja kwa moja kwenye round ya kwanza lakini hakutamzuia kuongoza uchaguzi huu (kwa maoni yangu).

...Ni kupata 25% ya kura ambazo atazipata tu, hofu ni kigezo cha kupata 50% ya kura zote, kuna uwezekano pia wa kupata chini ya 50% na hivyo uchaguzi kurudiwa..
 
Ndugu yangu hicho bado ni kitendawili ambacho sijajua kama kitateguliwa kwa urahisi. Tusubiri tuone mambo yatakuwaje ingawaje kwa matokeo ya hivi karibuni, Raila ameanza kupanda wakati Uhuru anashuka. Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, kupanda kwa Raila kunaweza tu kumzuia Uhuru asipite moja kwa moja kwenye round ya kwanza lakini hakutamzuia kuongoza uchaguzi huu (kwa maoni yangu).

Tiba

Hata kwa tathmini yangu naona Kenyatta ataongoza ila sikuwa na uhakika wa yeye kushinda round ya kwanza.Kitu cha ajabu sana ambacho hakikutarajiwa na wengi ni kuanguka kwa washindani wengine na kusabibisha uchaguzi kuonekana wa watu wawili.Nilitegemea hawa wengine watafanya vizuri Maeneo yao.Inashangaza mtu kama Keneth hajafikisha hata 30,000 ya kura!
 
friends of raila!sound kama friends of simba!!
 
Wamesema Raila ameshinda kwa kura mil 6.7 na uhuru kapata mil 5.2
 
Hata kwa tathmini yangu naona Kenyatta ataongoza ila sikuwa na uhakika wa yeye kushinda round ya kwanza.Kitu cha ajabu sana ambacho hakikutarajiwa na wengi ni kuanguka kwa washindani wengine na kusabibisha uchaguzi kuonekana wa watu wawili.Nilitegemea hawa wengine watafanya vizuri Maeneo yao.Inashangaza mtu kama Keneth hajafikisha hata 30,000 ya kura!

Huyu Kenneth zaidi zaidi anachukua kura ambazo zingechukuliwa na Uhuru. All in all kama ningekuwa ni Mkenya, ningempigia sana debe huyu Bwana kwa sababu kubwa mbili;

1. Anaonekana ni mtu mwenye msimamo na anazungumza kwa kujiamini. Angepewa nafasi, angeweza kupambana na ufisadi kwa nguvu zake zote.

2. Ni mtu mgeni ambaye hajajihusisha sana na siasa za Kenya za wakati uliopita kwa hivyo yeye angekuwa neutral kwenye serikali yake. Lakini hawa wengine, yeyote atakayechukua nchi, lazima kulipiza visasi kutachukua nafasi yake.

Hao wengine kina Mudavadi ni dhahiri walijua kwamba nafasi yao ni ndogo lakini lazima wahakikishe wanaingia kwenye historia ya Kenya kwamba waliwahi kugombea urais.

Tiba
 
Kwenye facebook na Radio za kenya friends of Raila Odinga wametangaza wazi kwamba bosi wao ameshinda nafasi ya Urais baada ya wao kujumlisha kura za nchi nzima za vituo vyote. Hii ndo habari mpya ya mchana huu. Hongera kwa Chadema waliomsapoti Odinga.
hii ndio mbaya sasa. friends kumtangaza mtu kama mshindi.
maaneke wafuasi woote wataamini kashinda.
tume ikija tangaza vinginevyo kasheshe inaanza!
 
Huyu Kenneth zaidi zaidi anachukua kura ambazo zingechukuliwa na Uhuru. All in all kama ningekuwa ni Mkenya, ningempigia sana debe huyu Bwana kwa sababu kubwa mbili;

1. Anaonekana ni mtu mwenye msimamo na anazungumza kwa kujiamini. Angepewa nafasi, angeweza kupambana na ufisadi kwa nguvu zake zote.

2. Ni mtu mgeni ambaye hajajihusisha sana na siasa za Kenya za wakati uliopita kwa hivyo yeye angekuwa neutral kwenye serikali yake. Lakini hawa wengine, yeyote atakayechukua nchi, lazima kulipiza visasi kutachukua nafasi yake.

Hao wengine kina Mudavadi ni dhahiri walijua kwamba nafasi yao ni ndogo lakini lazima wahakikishe wanaingia kwenye historia ya Kenya kwamba waliwahi kugombea urais.

Tiba

Keneth hata akikosa wakati huu naamini atakuja tena kuwa Rais wa Kenya,ana maono anafaa kuwa Command in Chief.
 
Odinga anakula 'vumbi' tu tangu kura zimeanza hesabiwa..hakuna cha friends of Odinga wala friends of Raila!
 
hivi kenya wana mgambo?. nasikia harufu ya damu kenya. mia
 
...Ebu angalia hizi Country, angalia matokeo ya hizo Country, angalia ngome za Uhuru, angalia Registered Votes, angalia kura zilizojumlishwa mpaka sasa, linganisha na ngome za Raila, alafu pata jibu....

...Nikupe mifano michachae...

1. Baringo: Uhuru ana 88%
Odinga ana 10%
Kura zilizojumlishwa mpaka sasa ni kama 75,000; Jumla ya Wapiga kura hapo ni 548,000

2. Bomet: Uhuru 93%
Odinga 4%
Kura zilizojumlishwa mpaka sasa ni kama 105,000; Jumla ya Wapiga kura hapo ni 730,000

3.Marakwet: Uhuru 92%
Odinga 5%
Kura zilizojumlishwa mpaka sasa ni kama 16,000; Jumla ya Wapiga kura hapo ni 346,000

4.Laikipia: Uhuru 87%
Odinga 11%
Kura zilizojumlishwa mpaka sasa ni kama 72,000; Jumla ya Wapiga kura hapo ni 621,000

5.Nandi Uhuru 85%
Odinga 6%
Kura zilizojumlishwa mpaka sasa ni kama 80,000; Jumla ya Wapiga kura hapo ni 417,000

SOURCE: Website ya Tume ya Uchaguzi: Kenya Elections 2013 - Daily Nation

Ngoma bado mbichi sana tu.
 
Kwenye facebook na Radio za kenya friends of Raila Odinga wametangaza wazi kwamba bosi wao ameshinda nafasi ya Urais baada ya wao kujumlisha kura za nchi nzima za vituo vyote. Hii ndo habari mpya ya mchana huu. Hongera kwa Chadema waliomsapoti Odinga.

Redio kifua hiyo!
 
Back
Top Bottom