From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
hawa si ndo waandishi wanaosemwa wamenunuliwa na mafisadi ili kuchafua viongozi kwenye mitandao ya jamii?bado hawajajifunza tu kutoka kwa mwenzao moja aliyetumika vibaya kuchafua watu mitandaoni?muda utasema na sidhani kama kama mtu atapoteza muda kuusoma huo upuuzi wao waliouandika.sidhani hata kama hicho kitabu kitanunuliwa na hata huyo askofu aliyekizindua kitabu hicho namshangaa.mbona wezi wakubwa na mafisadi papa aliowahi kuwasema marehemu mengi hawajawahi kuandikiwa kitabu ili watz wawajue!leo wanamwona jpm ndo kafanya mabaya kuliko mijizi mikubwa iliyokuwa inatorosha nje fedha za watz!ama kweli nimeamini asali ni tamu sana mpaka inafanya midomo ya watu ifungwe kama vile imenaswa na ulimbo.
 
Ndio hisia zako zinavyokwambia hivyo? Halafu mie nilidhani huo uhuni wake ulikuwa hadharani kila mtanzania na dunia inajua kumbe sivyo, sasa mnamdananisha vp na Idd Amini na Hitler?

Unaongea nini dogo, mechi ya Simba na Yanga watu kibao tumeona mubashara, sasa hivi vyombo vya habari vinavyoendelea kutangaza habari zile ikiwemo matokeo ya mechi ile, ni ili iweje wakati ile mechi ilikuwa wazi na watanzania na dunia waliiona?
 
Ndugu usilalamike sana kuhusu Magu,najua alikutumbua na vyeti vyako fake,Mama kasema wote wenye vyeti fake anawarudisha tena kazini na ma fake yenu ili muendeleze tena usanii wenu wa upigaji!!
Hivi shujaa naye si alikuwa na cheti fake vya Ph.D. ambacho kilisababisha Ben Saanane kupotezwa baada ya kuhoji na kuchambua kwa kina? Watu wenye mapenzi mema hawakuchukizwa na zoezi la kuhakiki uhalali wa vyeti wanavyotumia waajiriwa wa sekta ya umma. Badala yake watu walichukizwa na undumilakuwili uliojitokeza. Katikati ya uhakiki huo zilijitokeza tuhuma za kughushi vyeti na majina lakini zikafumbiwa macho. Shujaa mwenyewe akapoteza uhalali wa kuendesha hilo zoezi ilipobainika kuwa naye shahada yake ya uzamivu kaikukidhi miongozo ya chuo kikuu kwa kutunukiwa ndani ya miaka 3 badala ya 5! Katika demokrasia ya kweli, hiyo ilikuwa kashfa kubwa na alipaswa kujiuzulu.
 
Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!

Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.

Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?

Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?

Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?

Mkapa na kusini?

JK?

Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?

Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.

Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
Historia ilishatengenezwa acha watu waandike yale wanayoona yanafaa ili kutunza historia.
 
Yaan watu wazima Tena wazee na akili zao wanapoteza muda mwingi kwa kufanya vitu vya kijijnga na kipumbavu.Ngurumo kwa umri ni Mzee ,lakin anafanya ujinga mwingi.Sijui maisha yake atayatengeneza lini.
Kunywa soda ya baridi ili akili zirudi.
 
Unaongea nini dogo, mechi ya Simba na Yanga watu kibao tumeona mubashara, sasa hivi vyombo vya habari vinavyoendelea kutangaza habari zile ikiwemo matokeo ya mechi ile, ni ili iweje wakati ile mechi ilikuwa wazi na watanzania na dunia waliiona?
Aisee! Ndio unaanza kuzeeka au vp? Sasa huo ndio mfano gani? Wewe umeniambia kuwa mie najiliza pale uhuni wa Magufuli unapowekwa hadharani kwa maana sitaki huo uhuni wa Magufuli kuwekwa hadharani nataka watu wasiujue ukweli huo, sasa matokeo ya simba na Yanga yapo hadharani teyari yanajulikana.
 
Matokeo ya Yanga na simba yanaendelea kutangazwa ya nini wakati tunayajua?
 
Matokeo ya Yanga na simba yanaendelea kutangazwa ya nini wakati tunayajua?
Hivi hauoni unatoka nje ya mada? Nimekwambia matokeo ya simba na yanga teyari yapo hadharani ,hivyo hao wanaotoa matokeo hawadai kuwa ndio wanaweka matokeo hadharani.
 
Hivi hauoni unatoka nje ya mada? Nimekwambia matokeo ya simba na yanga teyari yapo hadharani ,hivyo hao wanaotoa matokeo hawadai kuwa ndio wanaweka matokeo hadharani.

Narudia tena, kitabu kinaweka wazi matendo ya dhalimu, kwa anayejua kinakazia na asiyejua anajulishwa. Una hoja nyingine?
 
Inatusaidia nn kuyajua?
HAMKUSEMA MWANZO MSISEME MILELE!
 
Alikuwa anafelifeli sana
Wote waliofeli mara nyingi na ambao hawakukata tamaa kwenye kurudia kwao na kujaribu ndo the most succesful people hivi sasa... Soma historia ya Shein, Ben Carson.... n.k Kama unapenda burudani soma historia ya Michael Jordan au Harry kane.

Humu kwenye fani ya taaluma ndo wapo tele! Serikalini wamejaa!
 
Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!

Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.

Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?

Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?

Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?

Mkapa na kusini?

JK?

Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?

Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.

Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
Inatakiwa tujifunze kutokana na makosa.

Mpaka leo hadithi za Iddi Amini au Adolf Hitler zinaongelewa kila kukicha.

Magufuli ni funzo ambalo watanzania wanatakiwa wajifunze miaka 500 ijayo.
 
Narudia tena, kitabu kinaweka wazi matendo ya dhalimu, kwa anayejua kinakazia na asiyejua anajulishwa. Una hoja nyingine?
Ni vichekesho tu, yani katika njia zote mlizotumia hazijafanikiwa ndio mkaona kitabu ndio njia sahihi kwa kumuhabarisha muafrika tena mtanzania? Labda mjikumbushe na kujifurahisha wenyewe kwa wenyewe.
 
Inatakiwa tujifunze kutokana na makosa.

Mpaka leo hadithi za Iddi Amini au Adolf Hitler zinaongelewa kila kukicha.

Magufuli ni funzo ambalo watanzania wanatakiwa wajifunze miaka 500 ijayo.
Duh miaka 500 ijayo kwa lipi tena mnamfananisha na Hitler.
 
Back
Top Bottom