From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.
Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.
Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo kuelekezwa huko kwa matakwa yake.
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.
Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.
Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.
Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Watakinunua bavicha
 
Magufuli angekuwa mzembe sana kama angefanya maendeleo kwengine kisha angeacha kwao. Yaani siku angestaafu angerudi kwao angestahili kupigwa mawe.

Lakini asingefanya ingembidi mwisho wa siku na yeye amlilie rais apeleke barabara, hospital, maji, shule na umeme. Vinginevyo ingebidi aikimbie chato kama Mkapa alivyoikimbia Masasi, Nyerere alivyoikwepa Butiama na kuishi msasani, Mwinyi alivyoikwepa mkuranga na kuishia mikocheni na Kikwete anavyoikwepa Msoga na kuishi dar au USA ili kuinjoy huduma za kijamii na maisha bora.

Kuhusu kauli ya watch out ni onyo ambalo Magu alilitoa kwa walioonekana kutaka kutishia amani. Kumbe kwao neno lile ilikuwa onyo tosha la kuiacha nchi itawalike na maendeleo yafanyike. Safi sana.

Lakini nawashauri pia waandishi watembee mikoa mingine waangalie Magu alifanya nini. Wasiishie Chato. Tena wangeanzia tu dar hususani maeneo ya Tandale, buza, manzese, temeke, mbagala, buguruni.
Hakuna maendeleo yoyote kwa wakazi wa Chato, ndio tunaweza kusema maisha kwasasa yamekuwa magumu zaidi.
 
Umekisoma na kukielewa kipande hiki?

"Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao."

Hiki kitabu hajaandikiwa Magufuli. Magufuli kashakufa.

Hiki kitabu wameandikiwa waliobaki. Wasiharibu kama alivyoharibu Magufuli. Wakiharibu watachafua legacies zao.
Ila wamemkamia mtu ambaye harudi Tena badala wa focus na future na mambo ya muhimu wao mara chato mara magufuli inachosha
 
Hawajamkamia. It is the life he chose.

Magufuli mwenyewe kaamua kuingia kwenye maisha ya siasa, hajalazimishwa na mtu.

Ukishaamua kuwa mwanasiasa, kuongoza mamilioni ya watu, umeamua kuacha maisha ya privacy, umekubali watu wayachambue maisha yako vizazi na vizazi.

Angeamua kuwa private citizen kama mimi, kusingekuwa na mtu anayemuandika.

It's the price of admiralty.
 
Nitakinunua nione mtazamo wa walamba asali kwa Mzalendo wa kweli, Hayati John Magufuli.
Hakika Mungu Yu mwema Kwa kumleta Rais mpenda haki mama Samia,Mungu aliona taifa linaangamia kwa ushamba,ulimbukeni,majivuno,umungu mtu,mauaji,ukabila,ukanda,na ulimbukeni uliotukuka hakika Mungu wewe ni muweza!! Hukukose
 
Magufuli angekuwa mzembe sana kama angefanya maendeleo kwengine kisha angeacha kwao. Yaani siku angestaafu angerudi kwao angestahili kupigwa mawe.

Lakini asingefanya ingembidi mwisho wa siku na yeye amlilie rais apeleke barabara, hospital, maji, shule na umeme. Vinginevyo ingebidi aikimbie chato kama Mkapa alivyoikimbia Masasi, Nyerere alivyoikwepa Butiama na kuishi msasani, Mwinyi alivyoikwepa mkuranga na kuishia mikocheni na Kikwete anavyoikwepa Msoga na kuishi dar au USA ili kuinjoy huduma za kijamii na maisha bora.

Kuhusu kauli ya watch out ni onyo ambalo Magu alilitoa kwa walioonekana kutaka kutishia amani. Kumbe kwao neno lile ilikuwa onyo tosha la kuiacha nchi itawalike na maendeleo yafanyike. Safi sana.

Lakini nawashauri pia waandishi watembee mikoa mingine waangalie Magu alifanya nini. Wasiishie Chato. Tena wangeanzia tu dar hususani maeneo ya Tandale, buza, manzese, temeke, mbagala, buguruni.
Kwahiyo Nyerere alikuwa mzembe!?qmmmco
 
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.
Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.
Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo kuelekezwa huko kwa matakwa yake.
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.
Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.
Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.
Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Ila mambo yanatofautiana, watu wachache kupiga zaidi ya 30T kila mwaka peke yako na kujenga miradi mikubwa inayotumiwa na watanzania wote kipi bora?
 
Kwa wazoefu wanajua kabisa nn kinaachwa kwenye makaratasi kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom