From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Mliambiwa chato ilakuwa kama Gbadolite kijiji Cha Mobutu paka wakabisha haya Sasa!! Asante Mungu
Nimeenda Chato kabla na baada ya kifo cha JPM, the township is growing into a full fledged town, just like any urban Tznian town, achana na propaganda za jf. He laid the foundation the rest is history, kuna nightlife na vibe kama ya miji mingine midogo yenye hadhi ya wilaya na huwezi boreka,
 
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.
Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.
Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo kuelekezwa huko kwa matakwa yake.
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.
Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.
Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.
Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Paka ameodoka mapanya wameanza kuja hata sebureni
 
Wapuuzi tu.kwa hiyo walitaka chato isijengwe?kama hawataki chato ijengwe wangeikataa ili iwe sehemu ya rwanda au burundi.yaani wanataka kuwabaguwa watz wa chato ili wasipate huduma za kijamii?Nani anunue hiyo takataka
 
Hao waandishi wanatafuta hela labda na umaarufu. Kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea nakosa lugha nzuri ya kuita kitendo hiko. Labda atokee mtu mwingine wa kuandika kitabu kwa yale mazuri aliyofanya JPM,ni fursa pia. Maiti asipoweza kujitetea walio hai wamsemee.
Matendo na tabia ya mtu ndio utetezi tosha. Tujitahidi tuache mambo na matendo yetu mazuri ili ziwe stori nzuri kwa vizazi na vizazi. Mfano Nelson Mandela
 
Hata na Mimi ningeangalia kwetu tuacheni unafiki uchwara au vp wakuu?hahahaaaaa..... Nimewaza tu Kwa sauti sijasema.....
 
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.
Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.
Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo kuelekezwa huko kwa matakwa yake.
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.
Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.
Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.
Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Pum..vu zenu ripoti ya Sasa ya CAG hamyaoni madudu? Kutwa kuanzisha news za kumponda JPM.
Mkome JPM atabaki Kuwa Rais bora Kuwahi tokea Tz.

Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app
 
Walinyamaza kimya wakati mwenyewe yuko hai. Jasiri ni wale waliopaza sauti akawasikia akasirika sana halafu wakapaza tena na tena.Wengine walifungwa,waliumizwa wakapewa kesi feki,wengine walinyang'anywa leseni zao za kazi za uwakili,Wengine biashara zao ziliharibiwa,wengine walidhurumiwa kwa nguvu kwenye uchaguzi n.k.Hao ni wazalendo wenye misimamo thabiti.Huwa nawadharau sana wale wanaompigaga risasi "nyati aliyekwisha kufa"

wakati hayo yanafanyika hao Waandishi wa habari walinyamaza kimya kabisa,vyombo vya habari vilinyamaza kimya kabisa.Wapo wachache sana wanaohesabika nawakumbuka waliopiga kelele.
 
Walikuwa wapigana vita gani ili ndio tumjue mshindi na mshindwa? Kama walikuwa wanapigana vita ya kuuwana basi hapo kweli JPM kashindwa.
Vita dhidi ya udikteta, na kweli udikteta na ukabila na chuki za kisiasa na kutekana na ukanda umekwisha kabisa. Sasa kama hawajashinda niambie JPM kashinda nni?
 
Mimi nawaulizeni nyinyi mnaosema mnauweka uchafu wake wazi huku mkijua keshaoza na hana impact, mkiambiwa achaneni nae basi keshafariki mnasema hata Hitler anasemwa. Kwahiyo kama mnajua hana impact keshaoza basi ndio muda wa kumpotezea haina haja ya kumpa nafasi kwenye majukwaa mitandaoni hadi na vitabu kabisa.
Sisi Chadema tulishamalizana na JPM tokea siku aanze kuoza pale Mzena. Haya mengine yote ni kuwafumbua waTanzania Ili asije tokea kiongozi wa aina yake (Bashiru, Sabaya, Kabudi, Makonda) kupewa nchi na Wala sio kumchafua. Hata Mama Samia ameshakiri kuwa Never, Never, and Never again kumpa Urais mtu wa calibre ya JPM.
 
Mambo ya uchaguzi ndio maana hata vyama vya upinzani vinashirikiana ili kupata kura nyingi ukichilia mbali na kuchukua watu kutoka ccm, mimi nazungumzia kilichopo mtaani Samia hakubaliki kama anavyokubaliki Jiwe, sasa hizo rekodi mlizoweka sawa ni rekodi mkuu?
Kama anakubalika why alivuruga uchaguzi? Mfano kata nayoishi mbunge alipita bila kupingwa, diwani pia alipita bila kupingwa kiufupi watu hatukupiga kura sababu walipita bila kupingwa. Sasa ndio Nini hiko? Alafu lijitu linakomaa eti anakubalika, Sasa aliogopa Nini upinzani kuweka wagombea?
 
Swali ambalo kila siku najiuliza, hivi ingekuaje kama Mungu angemuacha yule bindamu kuwa hai mpka leo hi?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kama Mungu angemuacha mpaka leo ingekuwa kama ifuatavyo;
1. Hadi sasa tungeshuhudia kwa mara ya kwanza TZ treni za mijusi zikikatiza kwenye SGR dar- moro - dom.
2. Upigaji wa trilioni zaidi ya 30 tusingeusikia.
3. Maharage tungekuwa tunachemshia umeme maana Nyerere dam ingekuwa imeisha na umeme ungekuwa bwerere.
4. Tungeshuhudia miradi mikubwa mno Tanzania kuwahi kutokea africa mashariki na kati.
 
Back
Top Bottom