mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 31,415
- 38,761
Mnangoja nini kuandika hicho kitabu cha mema yake, au nyie sio wabunifu bali ni watu wa kuiga tu baada ya wabunifu kuanzisha jambo?
Mema huwa hayatajwi,maana huwa yanaonekana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mnangoja nini kuandika hicho kitabu cha mema yake, au nyie sio wabunifu bali ni watu wa kuiga tu baada ya wabunifu kuanzisha jambo?
Hawa ni wapumbavu.. kwanini hawajaenda kuuliza imekuaje sumbawanga mjini kuna barabara safi na taa za pembezoni.. ?Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni
Ijumaa, Aprili 14, 2023
![]()
Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.
Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.
Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.
Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.
Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.
Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.
Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Waambie serikali wakifute basiHawa ni wapumbavu.. kwanini hawajaenda kuuliza imekuaje sumbawanga mjini kuna barabara safi na taa za pembezoni.. ?
Simba akizeeka kukimbilia waliko fisi.
Kwanza serikali ipige marifuku hiki kitabu..
Kwako ni mema, sisi tunaona ni wajibu wa serikali kupitia kodi za wananchi. Nenda Afrika kusini kama kuna mweusi yoyote anasema miundombinu iliyojengwa na makuburu ni wema. Usichanganye wema na wajibu. Angekuwa volunteer kisha afanye aliyofanya ungetamka neno wema.Mema huwa hayatajwi,maana huwa yanaonekana.
Tayari kitabu kiko sokoni kama vipi na nyie mifugo ya Magufuli andikeni kitabu cha kumpamba, simple!!!Hawa ni wapumbavu.. kwanini hawajaenda kuuliza imekuaje sumbawanga mjini kuna barabara safi na taa za pembezoni.. ?
Simba akizeeka kukimbilia waliko fisi.
Kwanza serikali ipige marifuku hiki kitabu..
Mwache Mungu aitwe MunguMnashindana ila hakika HAMTASHINDA.
Kwa hiyo yaliyofanyika wakati wa giza hutaki yasemwe?Wapumbavu badala ya ku deal na wizi wa sasa wa CAG wako Bize na marehemu tu ,naona group la ngurumo na meena hapo
USSR
Sent using Jamii Forums mobile app
Sukuma Gang hainaga brain hata kama ni ProfesaTayari kitabu kiko sokoni kama vipi na nyie mifugo ya Magufuli andikeni kitabu cha kumpamba, simple!!!
Umekisoma kitabu? Umejua maudhui yake? Isije ikawa hujasoma kisha unabweka? Issue kubwa ni kwamba raisi alipendelea alikozaliwa siyo kwamba hakujenga miradi hapana. Alipendelea kwao bila idhini ya bunge. Soma I am the stateHuo ni upambavu wa kiwango cha SGR na kuna mtu kawalipa.Waongee lingine, kwenye suala la miradi hapo wamechemka!
Reli ya SGR inaenda Chato?Mradi wa Umeme Rufiji upo Chato?Bandari kavu ya Kwala ipo Chato?Mradi Ujenzi wa mji Mkuu wa serikali upo Chato?Ujenzi wa vituo vya Afya zaidi ya 300 vipo Chato?Kijazi Flyover ipo Chato?Mfugale Flyover ipo Chato?Barabara ya njia nne Kimara mpaka Kibaha ipo Chato?
Kwa uchache,Waandishi wameongozwa na chuki zaidi ya uhalisia.
JK mwenyewe alipeleka umeme Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga ambapo hakuna mradi wowote bali Umeme alipata Mkwewe Baba yake na Salma na shambani kwa mkewe!
Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao alizindua mwaka 2014!
Inshort Kibanda na Ngurumo kama wamo humu jukwaani wajue wamejidharirisha akiwemo na Baba Askofu!.Ila Ngurumo nadhani stress za kukimbia nchi zinamsumbua!
Umchafue marehemu kisha uhongwe? Huyo mhongaji anapata nn?Waandishi wenyewe hao wanajulikana sio waadilifu ni watu wa madili. Wamehongwa kwenda kumchafua marehemu ili wapate ulaji. Majizi yanajuana
Kwanza nani kasema kuwa hicho ndio kipimo halisi? Kwa hoja zipi? Yani usionekane kukubalika mtaani halafu utuambie et kipimo cha kukubalika ni kwenye uchaguzi?Imebidi nicheke sana, awe anakubalika sana huko mtaani, ila ikifika kwenye kipimo halisi cha kukubalika kwake ashindwe kuheshimu zoezi hilo! Hii ni kali ya mwaka.
Ukiambiwa hao waliyokuwa wanaandika mazuri tu ni mashabiki zake au chawa waweke, je wewe unayeandika mabaya tu ni nani adui yake au unamchukia tu?Kumbe kweli alikuwa na mabaya, sasa kuna ubaya gani wa mtu kuandika mabaya yake tu? Nyie si mngejotikeza kuandika mazuri yake tu? Au ni hatua gani walichukuliwa waliokuwa wanaandika mazuri yake tu bila kuchanganya na hayo mabaya yake?
Mpaka leo wapo watafiti wanamtafiti yesu je nao ni wapumbavu? Usije ukawa we ndo mpumbavu kiongozi? Ni mpumbavu sababu hutaki kusikia usiyopenda kusikia juu ya mpumbavu mwenzio jpmWapumbavu badala ya ku deal na wizi wa sasa wa CAG wako Bize na marehemu tu ,naona group la ngurumo na meena hapo
USSR
Sent using Jamii Forums mobile app
Umekisoma kitabu mkuu?Historian ndo kitu gani? Huko Chato hakuna watu? Hayo maendeleo alopeleka hawastahili? Hebu kuweni na akili sometimes.
Kwako ni mema, sisi tunaona ni wajibu wa serikali kupitia kodi za wananchi. Nenda Afrika kusini kama kuna mweusi yoyote anasema miundombinu iliyojengwa na makuburu ni wema. Usichanganye wema na wajibu. Angekuwa volunteer kisha afanye aliyofanya ungetamka neno wema.
Ww deal na ripoti ya CAG, wengine wanadeal kuanika uchafu wa dhalimu.
Nadhani tufike mahali tuwe objective. Tukisome kitabu kisha tukichambue na kuona ninkwa kiasi gani kinawasilisha ukweli au vinginevyo. Tutaju ni kwa kiasi gani "I am the State" kinauzugumzia uzalendo wa mwendazake.Aachwe apumzike! Kama serikali ya SSH itaendelea kuruhusu udhalilishaji huu dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi mzalendo aliyetangulia mbele za haki basi wajue wanawakwaza watu wengi sana.