Kilimbatzz
JF-Expert Member
- Feb 11, 2023
- 9,134
- 14,593
Pamoja mkuuAl Merrikh ya Sudan wakitumia Uwanja wa Pele Kigali watawaalika Young Africans ya Tanzania katika mchezo wa mkondo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Africa.
Ni mchezo wa aina yake kwani Young Africans imefanikiwa kusafiri kwa kishindo cha mashabiki wengi mpaka jijini Kigali hivyo kuleta chache ya kuondoka na ushindi.
Tuwatakie heri na fanaka nyingi kwa Young Africans ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo.
Mechi itakuwa live saa 10:00 jioni na itakujia kupitia Azam Sports 1HD