FT: Algeria 0-0 Tanzania | AFCON Qualifier | Tanzania yafuzu AFCON

FT: Algeria 0-0 Tanzania | AFCON Qualifier | Tanzania yafuzu AFCON

Jamani jamani jamaaaani Uganda 2 huko.

Hawa taifa wakifungwa tu kwishaaaaaa
 
Mechi ya Dar es Salaam tulipowafunga wale vijana wa kurudisha mipira wakawa wanapoteza mda,mpira ulipoisha kocha wao kwa hasira akihojiwa alisema uhuni mliofanya mechi inayofuata tutamwachia Uganda atufunge halafu tuone mtafuzu vipi

Kumbe, tabia za kihuni huwa sizipendi kabisa ndani ya uwanja.
 
Mechi ya Dar es Salaam tulipowafunga wale vijana wa kurudisha mipira wakawa wanapoteza mda,mpira ulipoisha kocha wao kwa hasira akihojiwa alisema uhuni mliofanya mechi inayofuata tutamwachia Uganda atufunge halafu tuone mtafuzu vipi
Ah bc bora tufungwe tuu 😂
 
Kwanini unambeza Mzize?
Wala simbezi. Ila ni ukweli bado hana uzoefu wowote ule kwenye timu ya Taifa! Na pia hata kwenye timu yake ya Yanga siyo chaguo la kwanza la mwalimu Garmond.

Hivyo kwa kitendo chake cha kupewa nafasi ya kuanza kwenye timu ya Taifa, ni ushahidi tosha kama Taifa hatuna wachezaji wengi wenye ubora wa kushindana na wenzetu.
 
Mafanikio ya Simba na Yanga yanaletwa na wachezaji wageni.

Yanga bila kuchukuwa kipande cha As Vita fainali ya CAF tungekuwa tunaisikia tu.
Na huu ndiyo ukweli mchungu! Kama tumeshindwa kuwa na professional players wengi nje wa kuja kulisaidia Taifa kwenye mechi kama hizi, basi bora tukapunguza tu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye ligi yetu.
 
Back
Top Bottom