Nibandika bandua leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, pale miamba ya soka Afrika mnyama mkali mwituni wekundu wa msimbazi, watakapo karibishwa na matajiri wa Azam FC katika kuwania pointi 3 muhimu ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu!
Mara baada ya mnyama kutoshana nguvu na mtani wake wa jadi jumapili iliyopita na azam kukung'utwa 2-1 na KMc, leo watapata nafasi ya kujiuliza,
ngoma ni saa 1 kamili jioni hii!
Wanalunyasi karibuni, mwana kulitaka mwana kulipewa.
Nguvu moja.
=======
01' Mpira umeanza Benjamin Mkapa
08' Ayoub Lyanga anajaribu kutoka nje ya 18 lakini mpira unapaa juu ya lango la Simba
13' Kyombooooo, anakosa bao baada ya pasi nzuri kutoka kwa Okra
17' Azam wanafika kwenye lango la Simba, Kona. Simba wanasimama imara na kona haina madhara.
22' Simba wanacheza pasi nyingi kuelekea lango la azam, mikono ya Ahmada inawaokoa Azam.
23' Onyango anamdhibiti barabara mshambuliaji wa Azam, Prince Dube na kushindwa kufika kwenye lango la Simba akiwa na mpira.
31' Dube anapiga off target akiwa yeye na Manula
33' Azam wanapiga pasi za mipenyezo, Manula ana-slide na kuokoa jahazi
34' ⚽ Prince Dubeeeeee, bao safi na maridadi kutoka pembeni.. Manula anashindwa kufikia na kuzama nyavuni
39' Kipree, anajaribu mpira unatoka nje ya lango
42' Dube anapiga kichwa na mpira unapaa juu ya lango la Simba
44' Azam wanapoteza mpira, Kyombo anaunasa lakini anapiga fyongo
45+1' Half time