FT: Azam FC 2-1 Yanga SC | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | 17.03.2024

Mi napenda kula tuu. Kuliwa hapana
 
Mkuu kwa mujibu wenu yanga mpira ni magoli kwamba mradi timu imefungwa basi hiyo ni mbovu hakuna mjadala, hao kina ihefu na kagera sugar sie tuliwafunga na azam tulitoa draw, kwani walivyocheza na sie ni tofauti na walivyocheza na nyie au
Hapana sijamaanisha hivyo kaka.
Embu rejelea kunisoma tena utaelewa nini nalenga.
Simba mnatakiwa muimarishe kikosi hata uchezaji wenu ni wa papatupapatu kaka.
AbdelHak Benchika anawabeba kimbinu ila wachezaji hawakidhi ubora wa kocha.
Hata ushindi wenu wa kulazimisha sana.
Simba isiporekebisha kikosi na kufanya usajili mzuri Wallahi kaka nimefunga nipo palee hamtoboi.
 
Vigezo vya kuwa timu bora ni vipi mkuu, timu mbovu inaweza kweli kufika hatua ya robo fainali ya makundi klabu bingwa afrika, yani mfano nyie hiyo hatua mliyofika mtu aje awaambie kwamba timu yenu ni mbovu mtamuelewa kweli mkuu
 
Vigezo vya kuwa timu bora ni vipi mkuu, timu mbovu inaweza kweli kufika hatua ya robo fainali ya makundi klabu bingwa afrika, yani mfano nyie hiyo hatua mliyofika mtu aje awaambie kwamba timu yenu ni mbovu mtamuelewa kweli mkuu
Mkuu kuna vitu viwili vimewabeba mpaka ninyi kufika pale.
Kwanza mshukuru kundi mlilokuwepo mtu mgumu alikua Wydad japo nae wydad anapitia transition period kama Bayern Munich maana hata ligi yake haongozi sijui kwasasa.
Pili mshukuruni AbdelHaki Benchika.
Mifumo yake inawabeba sana aisee.
Embu ichukue Simba hii ifananishe na ile Simba inaongoza kundi Al Ahly akiwa ndani ya kundi kesha ipambanishe na hii.
Simba ile ilikua creative katika uchezaji na ilikua imekamilika kiufundi kila idara.
Simba ya sasa forward zako Jobe na Freddy utafika wapi kaka??
Wachezaji wengi washanoki hawa kina Kapombe,Chama,Tshabalala Mohammed,Saido Ntibazonkiza n.k n.k
Pia hamuna mbadala wa hao watu katika upande wa viungo na wing back ambao wana quality sawa na hao wachezaji.
Mathalan Yanga akiumia Lomalissa namuingiza Kibabage kama mbadala ambae anafikia kwa kiasi fulani kiwango cha Lomalissa.
We aumie Kapombe utamuweka nani mwenye quality inayomfikia Kapombe??
Kama hamtafumua kikosi na mkakiunda kipya na kutanua kikosi kaka tegemeeni BENCHIKA KUFUKUZWA MCHANA KWEUPEEE.
Wachezaji wamechokaa hawa.
 
Mkuu uliyoyaandika sidhani kama yanadhihirisha kuwa simba ni timu mbovu, ndio maana nikakuuliza vigezo vya timu kuwa mbovu ni vipi unasema tunabebwa na kocha sasa kocha naye si ni sehemu ya timu au, uliyoyaandika ni faults ndogo za timu ambazo zinatokana na form ya wachezaji tu ila si kwamba simba ni mbovu mkuu
 
Jamaa unaandika maneno mengi lakini pumba tupu. Sasa maana ya timu ni nini
Shida hautaki kuukubali ukweli.
Timu ni chemistry baina ya wachezaji na mkufunzi wa hao wachezaji wenyewe.
Ndio maana unaona hata ulaya kina Guardiola wanachagua wachezaji wataoendana na mfumo na kuachana na wachezaji ambao tayari washaisha.
Hii ndio ilikua point yangu.
Kuna muda mchezaji hakidhi hadhi ya kocha hiyo hufanya falsafa za kocha kuwa ngumu kwa timu.
Hakuna pumba isipokua unapingana na ukweli.
 
Mkuu tuseme umepatia.
Simba sio mbovu tuache muda uongee.
 
Ndio maana nimemuuliza nini maana ya timu?
 
Aaaah wapii huna lolote kwani sijaona comments zako baada ya comment yangu!?
We sema ulikua unavizia matokeo tuu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli nilikua buzzy mie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…