Muda mchache ujao, El Clasico inapigwa.
Ni Barcelona Vs Real Madrid katika mchezo muhimu wa La liga ambao utatoa picha ya mbio za ubingwa.
Ikumbukwe ni El Clasico ya mwisho kwa Carlo Ancelloti kabla ya ujio wa Xabi Alonso pale Real Madrid.
Ancelloti amefungwa mechi zote alizokutana na Barcelona huku pengo la point likiwa ni tofauti ya alama 4 huku ikibakia michezo minne tu kabla ya mechi ya leo.
Ungana nami kwa live updates…
==================
1’ Real Madrid wanaanza mpira kwa kasi
2’ Mbappe anafanyiwa faulo kwenye box, refa anasema penati
4’ Goaaaaaallllll Mbappe anafunga penati
5’ Barcelona 0-1 Real Madrid
7’ Real Madrid ni kama wanaitaka sana mechi ya leo
10’ Barcelona 0-1 Real Madrid
12’ Barca wameanza kuliandama lango la Real Madrid kama kawaida yao
14’ Mbappe anaweka goli la pili na kufanya ubao usome Barcelona 0-2 Real Madrid
15’ Lamine Yamal yuko chini
19’ Garcia anawapa goli 1 Barcelona
20’ Barcelona 1-2 Real Madrid
23’ Watoto wa Barcelona wamecharuka sasa
25’ Barcelona 1-2 Real Madrid
28’ Real Madrid wamepaki basi mapema sana, mchezo umetawaliwa na Barcelona
29’ Fade Valverde anapata kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Lamine Yamal