Heri ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ni jumapili tulivu, Mnyama Mkubwa Mwituni, Simba Sports atashuka dimbani dhidi ya wenyeji wake Bravos ya Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo wa kwanza, Simba akiwa nyumbani aliibuka na ushindi wa 1-0, je ataendeleza wimbi la ushindi?
Simba inazidi kuimarika hasa ikichagizwa na ongezeko la Mpanzu, huku ikiwa nafasi ya pili na alama 9 wakati wenyeji Bravo wakiwa nafasi ya 3 na alama 6. Ni mtanange wa kufa na kupona.
Ikumbukwe kuwa Bravos ameshinda mechi zake mbili akiwa nyumbani, huku Simba akitoka kushinda ugenini mechi iliyopita, patawaka moto!
Mechi itakuwa mubashara Saa 1:00 Usiku kwa masaa ya Afrika ya Mashariki.
Karibuni wote, mshuhudie wawakilishi sahihi wa kimataifa wasiotumia CALCULATOR wakielekea Robo Fainali kama ilivyoada yao!!
View attachment 3199863