FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Mpira una maajabu yake ,furahia ushindi leo .

Mimi naliogopa Vibe la mashabiki wa kule mechi hizi wanashangilia kama wehu au vichaaa na wachezaji wanakuja na familia zao uwanjani kama wanapigana Jihad kutetea familia na nchi huwa hawana mzaha.
Nimefurahia ndio maana nikaanza na kwa mkapa hatoki mtu✅
 
Tusiwatimue tuzidi kuwapa nafasi. Kama Kibu tungemtimua tungekuwa wapi sasa hivi?
 
Imagine unaenda kwa Mwarabu, halafu anakuchezesha saa nne usiku! Na lile libaridi la usiku! Ukijumlisha na rekodi mbovu mnapocheza mechi za ugenini!

Dah! Uwezekano wa kusonga mbele, utategemea tu majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Muhimu nimeilinda heshima ya Kwa Mkapa, ya huko uarabuni naona tuwaachie waarabu..
 
Kule Maroco ni pagumu ..... ukorofi waliofanya leo waarabu wataenda kuufanya kwao na watacheza mpira sana

Binafsi naipongeza Simba kwa kuwafunga mabingwa Africa but kule Maroco hawa waarabu wanabadilikaga na kuwa watu wengine .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…