FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Mpira una maajabu yake ,furahia ushindi leo .

Mimi naliogopa Vibe la mashabiki wa kule mechi hizi wanashangilia kama wehu au vichaaa na wachezaji wanakuja na familia zao uwanjani kama wanapigana Jihad kutetea familia na nchi huwa hawana mzaha.
Nimefurahia ndio maana nikaanza na kwa mkapa hatoki mtu✅
 
Kwa Mkapa hatoki [emoji736]

Ila sasa kwa margin hii ya magoli, nisiwe mnafiki hata kama mpira unadunda, tumeaga mashindano, kule kwao hiyo Ijumaa watatupiga goli nyingi.

Tujilaumu wenyewe kwakushindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani!!

Lakini pia tuna wachezaji wengi wa kigeni ambao wanakula hela ya bure tu. Sawadogo, Okrah, Ouatarra nk

Nashauri wote watimuliwe!!
Tusiwatimue tuzidi kuwapa nafasi. Kama Kibu tungemtimua tungekuwa wapi sasa hivi?
 
Imagine unaenda kwa Mwarabu, halafu anakuchezesha saa nne usiku! Na lile libaridi la usiku! Ukijumlisha na rekodi mbovu mnapocheza mechi za ugenini!

Dah! Uwezekano wa kusonga mbele, utategemea tu majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Muhimu nimeilinda heshima ya Kwa Mkapa, ya huko uarabuni naona tuwaachie waarabu..
 
Kule Maroco ni pagumu ..... ukorofi waliofanya leo waarabu wataenda kuufanya kwao na watacheza mpira sana

Binafsi naipongeza Simba kwa kuwafunga mabingwa Africa but kule Maroco hawa waarabu wanabadilikaga na kuwa watu wengine .....
 
Back
Top Bottom