FT: CAF Confederation Cup | Semi Finals | Young Africans SC 2-0 Marumo Gallants FC | Mkapa Stadium | 10/05/2023

FT: CAF Confederation Cup | Semi Finals | Young Africans SC 2-0 Marumo Gallants FC | Mkapa Stadium | 10/05/2023

Mabingwa wa Tanzania, Dar es Salaam Young Africans maarufu kama Yanga, jioni ya leo watashuka dimbani uwanja wa Benjamini Mkapa kupambana na timu ya Marumo Gallants ya kutoka Afrika ya Kusini katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho hatua ya kwanza

Mechi hiyo itayochezwa saa kumi ya jioni, itakuwa ni muhimu kwa Yanga kupata ushindi mzuri kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya marudiano

Nitakuwa nawe katika kufuatilia na kuhabarisha kile kitakachokuwa kinajiri kwenye dimba la Mkapa jioni hiyo

Mungu Ibariki Yanga, Mungu ibariki Tanzania

View attachment 2616696
Yanga hamna budi kufa kiumee.... Maana hawa jamaa kwao ni wa Bad..

All the best
 
Kwanini hamtaki kuuamini uwezo wa Yanga?

Kwanini kila timu ambayo inafungwa na Yanga nyie mnasema ni timu dhaifu?

Tumecheza hatua ya makundi tukazifunga timu kubwa kama TP Mazembe home n away lakini mkadai eti siyo Mazembe ya miaka ile.

Tumeifunga US Monastir hapa kwa mkapa lakini bado mmekuwa watu wa kuibeza Yanga, kwanini?
Kwanini hamtaki kuamini kwenye ukweli?

Uwezo wa Yanga tunaukubali lakini je timu pinzani zilikuwa na ubora gani?

Mlipopangwa tu na Rivers mashabiki mlianza kushangilia, unafikiri hilo lingewezekana kama mngepangwa na timu ngumu?

Angalia Simba ilipopangwa na Mamelody kila mtu alikuwa anaitabiria mwisho wake tena kwa magoli mengi, unafikiri kwasababu gani?

Hivi kweli Tp Mazembe unaiona ni timu kubwa ila imezidiwa na Yanga au ni timu iliyopotea kwasababu ya kukosa wachezaji wenye Quality?

Hata nikikuuliza leo, ni mechi gani kwako ambayo ilikuwa ngumu kati ya Rivers United na Tp Mazembe utasema ipi?
 
Makolo msi jitetee kwenye hili jukwaa.nila mabingwa tu
132445500.jpg
 
Back
Top Bottom