FT: CAFCL: Simba SC 1-1 Power Dynamos | Simba yafuzu Hatua ya Makundi

Kila la kheri SIMBA

Kila la kheri SINGIDA FG

NOTE; SIMBA mkifungwa hatutahuzunika Sisi YANGA tumeshinda Jana kwa hiyo mkaze buti mkifungwa kuwacheka kupo palepale.
Hafungwi mtu, hii ni Simba na hii ni Dar es Salaam
 
Dynamo 3 Simba 1
Hongereni sana watani kwa kuvunja mwiko wa miaka 25 na kutinga makundi ya Klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. Ni jambo kubwa sana kwa wana Uto wote. Mnastahili pongezi. Japo mmeingia kwa kuwatoa wakimbizi lakini si mbaya.

Sisi tumezoea kuingia makundi kwa miaka mingi. Ni vitu vya kawaida kwetu. Lakini kwenu huu ni muujiza. Kidogo mlikua mnaliwezea lile kombe la "Loser" lakini huku kwenye klabu bingwa mlikuwa mnatepeta mapema sana. Mmekua "sokomoko" kwa miaka 25. Hatimaye leo mmevunja mwiko. Japo sijui ni upi maana mnapenda kusema "mbele mwiko nyuma mwiko" lakini nachojua mwiko mmoja umevunjika leo baada ya miaka 25. Hongereni sana.

Mara ya mwisho kufika makundi klabu bingwa ni 1998 wakati Mayele akiwa na miaka minne, Feitoto alikua mimba, na Whozu alikuwa na mwaka mmoja lakini leo anaitwa Chibaba [emoji1787]. Makundi pekee mliyokua mnaingia mara kwa mara ni ya Whatsapp. Kwahiyo hongereni sana kwa kuvunja mwiko.

Ilikua inatia simanzi sana wakati Simba tukienda group stage, nyie mnarudi kuosha vyombo na Njombe Mji au Itilima FC. Lakini mwaka huu ni furaha kwamba kaka zenu tumepata watu wa kutusindikiza kwenye makundi ya klabu bingwa. Raha mliyoipata leo, sisi tumeipata mfululizo kwa miaka mingi.

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Uto, hasa wenye umri chini ya miaka 25 hawajawahi kuishuhudia klabu yao ikicheza makundi klabu bingwa. Na walikua na hatari ya kuzeeka bila kuiona timu yao ikitinga hatua ya makundi. Kwahiyo leo wana haki ya kufurahi, kujibaraguza na hata kuogea maji ya bahari kwa kutoa mkosi.

Mwisho niwashauri vijana mnaotaka kuoa changamkieni mabinti ambao ni mashabiki wa Uto. Kama ameweza kuivumilia timu yake kwa miaka 25, hashindwi kukuvumilia wewe na chumba chako kimoja kwa miaka mitano mpaka utakapojenga kwako. Kuanzia kesho kama unatafuta mke "piga sound" binti yeyote aliyevaa kitop cha kijani na shimizi ya njano. Mtanishukuru baadae [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtani nakutakia kila la heri na mafanikio, ila hii so mechi rahisi, angalien game ya kwanza ya Yanga na jana jamaa walivyokaza..

Hala muelekezeni yule msemaji wenu aache maneno mengi, atawaponza kwa kuwapa matumaini hewa yasiyo na ukweli.

Bado kuna mambo yakufanyiwa kazi Simba, tena mengi tu, angepunguza maneno yasiyo maana na ku i promote yanga kila siku.

Mtani nakutakia mafanikio...
Dynamo Watake watafungwa, wasitake watafungwa ..
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Simba SC 3-1 Power Dynamos

Leo ndo majibu yatakavyokuwa ..

Ila naweza nikapunguza kidogo ikawa

Simba SC 2-1 Power Dynamos

Kulingana na ushindani ulivyo sasa hivi
Au ikiwa power watakuwa na defensive team sana...

Simba SC 1-0Power Dynamos

Tunzeni haya majibu
Hapo Sasa hayo magoli geuza kulia-Kushoto Mechi imeisha hiyo
 
Hongereni sana watani kwa kuvunja mwiko wa miaka 25 na kutinga makundi ya Klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. Ni jambo kubwa sana kwa wana Uto wote. Mnastahili pongezi. Japo mmeingia kwa kuwatoa wakimbizi lakini si mbaya.

Sisi tumezoea kuingia makundi kwa miaka mingi. Ni vitu vya kawaida kwetu. Lakini kwenu huu ni muujiza. Kidogo mlikua mnaliwezea lile kombe la "Loser" lakini huku kwenye klabu bingwa mlikuwa mnatepeta mapema sana. Mmekua "sokomoko" kwa miaka 25. Hatimaye leo mmevunja mwiko. Japo sijui ni upi maana mnapenda kusema "mbele mwiko nyuma mwiko" lakini nachojua mwiko mmoja umevunjika leo baada ya miaka 25. Hongereni sana.

Mara ya mwisho kufika makundi klabu bingwa ni 1998 wakati Mayele akiwa na miaka minne, Feitoto alikua mimba, na Whozu alikuwa na mwaka mmoja lakini leo anaitwa Chibaba [emoji1787]. Makundi pekee mliyokua mnaingia mara kwa mara ni ya Whatsapp. Kwahiyo hongereni sana kwa kuvunja mwiko.

Ilikua inatia simanzi sana wakati Simba tukienda group stage, nyie mnarudi kuosha vyombo na Njombe Mji au Itilima FC. Lakini mwaka huu ni furaha kwamba kaka zenu tumepata watu wa kutusindikiza kwenye makundi ya klabu bingwa. Raha mliyoipata leo, sisi tumeipata mfululizo kwa miaka mingi.

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Uto, hasa wenye umri chini ya miaka 25 hawajawahi kuishuhudia klabu yao ikicheza makundi klabu bingwa. Na walikua na hatari ya kuzeeka bila kuiona timu yao ikitinga hatua ya makundi. Kwahiyo leo wana haki ya kufurahi, kujibaraguza na hata kuogea maji ya bahari kwa kutoa mkosi.

Mwisho niwashauri vijana mnaotaka kuoa changamkieni mabinti ambao ni mashabiki wa Uto. Kama ameweza kuivumilia timu yake kwa miaka 25, hashindwi kukuvumilia wewe na chumba chako kimoja kwa miaka mitano mpaka utakapojenga kwako. Kuanzia kesho kama unatafuta mke "piga sound" binti yeyote aliyevaa kitop cha kijani na shimizi ya njano. Mtanishukuru baadae [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂😂😂
 
Wazambia wanafungwa wana makosa mengi sana kuliko Simba ile mechi ya kwanza walikoswa goli nyingi tu hawana mipango ya kutafuta goli na ukiona hayo magoli yao mawili yote ni ya kubahatisha tu Simba waanzisheni Miksoni na Kanoute akae benchi anafanya kiungo kinakua kigumu sana..
 
Mmecheza na timu iliyoteuliwa kushiriki mashindano mnajiona mmepiga mpira mwingi.subiri badae uone mech kamiki ya timu za mpira sio bonanza la ujirani mwema mlilocheza jana.
Galaxy walikua wateuliwa ila walitoa mtu ulimi
 
Back
Top Bottom