tamsana
JF-Expert Member
- Jan 13, 2012
- 3,739
- 8,044
Mkuu kwa hiyo kipimo cha ubovu wa simba unakopima kwa kuangalia uto!Simba ni mbovu! Kama wachezaji hawajitumi basi uongozi una shida! Na kama kuna fitna za upande wa pili wa utopolo basi uongozi wa Simba ni mbovu hauna uwezo wa kupambana na fitna za soka la Tanzania!
Simba ya Dalali, Simba ya Rage! Simba ya Kaburu! Simba ya malkia wa nyuki zote hizo zilikuwa Simba za misukosuko ila hazijawahi kufungwa tano na utopolo! Bali Simba ndio ilikuwa inapambana haswa!
Hakuna Simba iliyokuwa mbovu kama ya 2013! Ilikuwa ya vijana wa waliotoka Simba b! Ilikutana na yanya iliyokuwa vizuri kila idara ikiwa chini ya bilionea Manji,ila mechi ya tarehe 20 Oct 2013 Simba ilipata sare ya tatu tatu na yanga tena Simba ikitoka nyuma na kusawazisha goli zote mpaka yanga wakiomba mpira uishe!
Eti Simba inakuja kufungwa tano na yanga halafu linakuja shabiki la mchongo linasema Simba sio mbovu!
Timu inacheza na kupata ushindi wa kubahatisha halafu mtu anasema Simba sio mbovu!
Basi sawa.