Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB ni Derby ya Mzizima
Simba SC dhidi ya AzamFC
Mtanange huu unapigwa Jumamosi hii, Julai 04 katika dimba la Gombani Pemba, Saa 11:00 Jioni.
Mechi 5 za mwisho kati ya Simba SC na Azam FC kwenye Ligi Kuu:
5 Aprili 2026: Azam FC 0–0 Simba SC
7 Desemba 2025: Simba SC 0–2 Azam FC
24 Februari 2025: Simba SC 2–2 Azam FC
26 Septemba 2024: Azam FC 0–2 Simba SC
9 Mei 2024: Azam FC 0–3 Simba SC
Safu ya Waamuzi
Mwamuzi wa Kati wa mchezo wa Fainali ya CRDB CUP ni Sifu Amon kutoka Mbeya, Msaidizi namba moja ni Hamdan Said wa Mtwara, Msaidizi namba mbili ni Zawadi Yusuph Kutoka Dar es Salaam na Mwamuzi wa akiba ni Ahmed Arajiga wa Manyara.
Kikosi cha Simba SC
Kikosi cha Azam FC kimeingia uwanjani kikiwa kimesheheni idadi kubwa ya wachezaji wazawa kutoka Tanzania, jambo linaloonyesha imani kubwa kwa vipaji vya nyumbani katika mchezo huu muhimu dhidi ya Simba SC.
Wachezaji wazawa wanatawala kwa kuanza kuanzia golini na mlinda mlango Aishi Manula, akisaidiwa na safu imara ya ulinzi na viungo inayoundwa na Lusajo Lawi, Himid Mkami, Pascal Msindo, nahodha Lameck Mwaikenda, Iddy Nado, Feisal Salum, pamoja na washambuliaji Abdul Suleiman 'Sopu' na Yahya Zayd.