FT: France 2-0 Morocco | World Cup 2026 | Gillette Stadium | Julai 9, 2026 | 5:00 Usiku | Morocco kazi imeshia hapa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa robo fainali.

Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappé pamoja na Ousmane Dembélé, ushindi ambao umeihakikishia Les Bleus nafasi ya kuendelea na mbio za kuwania taji la dunia
=================
Marudio ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 yanatarajiwa kushuhudiwa jijini Boston, ambapo mabingwa watarajiwa Ufaransa watakutana na nguvu kubwa ya soka la Afrika, Morocco, huku kila timu ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Ufaransa imekuwa na safari nzuri katika michuano hii, ikishinda mechi zake nne za kwanza kwa kutegemea safu yake kali ya ushambuliaji yenye nyota wengi. Hata hivyo, katika hatua ya 16 bora walilazimika kupambana hadi mwisho ili kuibuka na ushindi mwembamba wa mabao 1-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Kwa upande wa Morocco, waliendelea kuonyesha ubora wao baada ya kuifunga wenyeji Canada mabao 3-0 katika hatua ya 16 bora. Licha ya kuwa na mashuti manne pekee yaliyolenga lango, walikuwa makini sana kutumia nafasi zao na kufuzu kwa kishindo.

Historia ya Kukutana (Head to head)​

Ufaransa haijawahi kupoteza dhidi ya Morocco katika mikutano yao sita iliyopita, ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare mbili. Ushindi wao pekee wa mashindano rasmi dhidi ya Morocco ulipatikana kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 waliposhinda mabao 2-0.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu zaidi kwa Ufaransa katika michuano hii, huku Morocco wakionekana kuwa wapinzani wenye uwezo wa kuandika historia nyingine kwa soka la Afrika
 
Morocco wanyoosheni hao wazungu hadi waseme nani kawapaka masizi.
Ngoja wazungu weusi wakuijie na marugu why uwaseme vibaya ndugu zao ufaransa huku wakiwakataa morocco 🇲🇦 timu inayotuwakilisha na ndio tumaini letu wana Afrika.

Kweli ubaguzi na chuki hautaisha. Kuna waafrika wapo tayari kuishabikia ufaransa iliyomuuwa Gadafi na kuitosa timu kutoka afrika Morocco, ni vichekesho. Hiyo hiyo the country ilihalalisha ushoga.

Kila la kheri Morocco 🇲🇦 ♥
 
Mechi ya Ufaransa dhidi ya Morocco ni robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 na itachezwa leo saa 23:00 kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Mshindi atafuzu hatua ya nusu fainali.

Kwa mtazamo wa ubora wa vikosi:
Ufaransa inaonekana kupewa nafasi kubwa zaidi kutokana na kikosi chenye uzoefu na wachezaji kama Kylian Mbappé, huku ikiwa imeshinda mechi zake zote hadi sasa kwenye mashindano.

Morocco imeonyesha uimara mkubwa wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza, ikiwa imewatoa wapinzani wakubwa na kutinga robo fainali kwa mafanikio makubwa. �
Houston Chronicle +1
Utabiri wangu wa mchezo huu ni:
Ufaransa 2–1 Morocco, lakini ikiwa Morocco itadhibiti mashambulizi ya Ufaransa mapema, mechi inaweza kwenda hadi muda wa nyongeza
 
Nafikiri Morocco wakijitahidi kukaa na mpira wanaweza kupata matokeo, kumbuka kule mbele France sio wakabaji wazuri, Morocco timu Yao yote iko aggressive kwenye man to man combat...wakimruhusu France akae na mpira muda wote basi atachapika maana France wanao watu wanaoweza kupiga pasi hatarishi zinazoweza kuvunja mstari wa ulinzi wa Morocco hasa Olise, licha ya kwamba anaweza kupata goli Kwa counter attacks....
 
Ngoja wazungu weusi wakuijie na marugu why uwaseme vibaya ndugu zao ufaransa huku wakiwakataa morocco 🇲🇦 timu inayotuwakilisha na ndio tumaini letu wana Afrika.

Kweli ubaguzi na chuki hautaisha. Kuna waafrika wapo tayari kuishabikia ufaransa iliyomuuwa Gadafi na kuitosa timu kutoka afrika Morocco, ni vichekesho. Hiyo hiyo the country ilihalalisha ushoga.

Kila la kheri Morocco 🇲🇦 ♥
Well said.
 
Nafikiri Morocco wakijitahidi kukaa na mpira wanaweza kupata matokeo, kumbuka kule mbele France sio wakabaji wazuri, Morocco timu Yao yote iko aggressive kwenye man to man combat...wakimruhusu France akae na mpira muda wote basi atachapika maana France wanao watu wanaoweza kupiga pasi hatarishi zinazoweza kuvunja mstari wa ulinzi wa Morocco hasa Olise, licha ya kwamba anaweza kupata goli Kwa counter attacks....
Ufaransa wazee wa counter attack, sisi wa morocco pira letu la spain/Argentina, pasi nyingi hahaaa, Kila la kheri kwao
 
Back
Top Bottom