Kombe la dunia linarudi palepale kwa wenyewe yaani Ulaya na Amerika Kusini na Ulaya kama kawaida anaingizaga timu nyingi katika hatua kama hii.
World Cup 2026 Ulaya imeingiza timu 6 kwenye hatua ya robo fainali Belgium, England, France, Norway, Spain na Switzerland wakati Amerika Kusini kaingiza timu moja tu safari hii ambayo ni Argentina na Afrika ni moja tu Morocco.
Tayari nusu fainali Ulaya ina uhakika wa kuingiza timu 3 na endapo Argentina itakwama kwa Switzerland basi itakua ni "The all European semi final" and final na itathibitisha ukweli kwamba kwa Ulaya huu mchezo sio kwamba ni kazi tu bali ni jadi yao kama Afrika tunavyo penda ngoma.
Ukitaka kujua kwamba Ulaya soka ni jadi angalia wanavyocheza mpira wa kushambulia badala ya huu wetu wa kiafrika wa kupaki basi tukijidanganya kwamba tunaweza kushinda bila kushambulia goli la adui.