Marudio ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 yanatarajiwa kushuhudiwa jijini Boston, ambapo mabingwa watarajiwa Ufaransa watakutana na nguvu kubwa ya soka la Afrika, Morocco, huku kila timu ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.
Ufaransa imekuwa na safari nzuri katika michuano hii, ikishinda mechi zake nne za kwanza kwa kutegemea safu yake kali ya ushambuliaji yenye nyota wengi. Hata hivyo, katika hatua ya 16 bora walilazimika kupambana hadi mwisho ili kuibuka na ushindi mwembamba wa mabao 1-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Kwa upande wa Morocco, waliendelea kuonyesha ubora wao baada ya kuifunga wenyeji Canada mabao 3-0 katika hatua ya 16 bora. Licha ya kuwa na mashuti manne pekee yaliyolenga lango, walikuwa makini sana kutumia nafasi zao na kufuzu kwa kishindo.
Historia ya Kukutana (Head to head)
Ufaransa haijawahi kupoteza dhidi ya Morocco katika mikutano yao sita iliyopita, ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare mbili. Ushindi wao pekee wa mashindano rasmi dhidi ya Morocco ulipatikana kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 waliposhinda mabao 2-0.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu zaidi kwa Ufaransa katika michuano hii, huku Morocco wakionekana kuwa wapinzani wenye uwezo wa kuandika historia nyingine kwa soka la Afrika