Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mechi ni kesho mkuu.Azama wameishia hapo kwenye mtoano? Maana mpaka sasa ni kimya
Mechi ni kesho sio leoAzama wameishia hapo kwenye mtoano? Maana mpaka sasa ni kimya
Ngoja wazungu weusi wakuijie na marugu why uwaseme vibaya ndugu zao ufaransa huku wakiwakataa morocco 🇲🇦 timu inayotuwakilisha na ndio tumaini letu wana Afrika.Morocco wanyoosheni hao wazungu hadi waseme nani kawapaka masizi.
Ngoja wazungu weusi wakuijie na marugu why uwaseme vibaya ndugu zao ufaransa huku wakiwakataa morocco
Hawa majamaa walivyokuwa wabaguzi ufaransa atasoma namba awe makiniInashangaza sana Marefa wote wa hii gemu ni kutoka Argentina.
Mechi ya Ufaransa dhidi ya Morocco ni robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 na itachezwa leo saa 23:00 kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Mshindi atafuzu hatua ya nusu fainali.Marudio ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 yanatarajiwa kushuhudiwa jijini Boston, ambapo mabingwa watarajiwa Ufaransa watakutana na nguvu kubwa ya soka la Afrika, Morocco, huku kila timu ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.
Ufaransa imekuwa na safari nzuri katika michuano hii, ikishinda mechi zake nne za kwanza kwa kutegemea safu yake kali ya ushambuliaji yenye nyota wengi. Hata hivyo, katika hatua ya 16 bora walilazimika kupambana hadi mwisho ili kuibuka na ushindi mwembamba wa mabao 1-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Kwa upande wa Morocco, waliendelea kuonyesha ubora wao baada ya kuifunga wenyeji Canada mabao 3-0 katika hatua ya 16 bora. Licha ya kuwa na mashuti manne pekee yaliyolenga lango, walikuwa makini sana kutumia nafasi zao na kufuzu kwa kishindo.
Historia ya Kukutana (Head to head)
Ufaransa haijawahi kupoteza dhidi ya Morocco katika mikutano yao sita iliyopita, ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare mbili. Ushindi wao pekee wa mashindano rasmi dhidi ya Morocco ulipatikana kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 waliposhinda mabao 2-0.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu zaidi kwa Ufaransa katika michuano hii, huku Morocco wakionekana kuwa wapinzani wenye uwezo wa kuandika historia nyingine kwa soka la Afrika
Well said.Ngoja wazungu weusi wakuijie na marugu why uwaseme vibaya ndugu zao ufaransa huku wakiwakataa morocco 🇲🇦 timu inayotuwakilisha na ndio tumaini letu wana Afrika.
Kweli ubaguzi na chuki hautaisha. Kuna waafrika wapo tayari kuishabikia ufaransa iliyomuuwa Gadafi na kuitosa timu kutoka afrika Morocco, ni vichekesho. Hiyo hiyo the country ilihalalisha ushoga.
Kila la kheri Morocco 🇲🇦 ♥
Ufaransa wazee wa counter attack, sisi wa morocco pira letu la spain/Argentina, pasi nyingi hahaaa, Kila la kheri kwaoNafikiri Morocco wakijitahidi kukaa na mpira wanaweza kupata matokeo, kumbuka kule mbele France sio wakabaji wazuri, Morocco timu Yao yote iko aggressive kwenye man to man combat...wakimruhusu France akae na mpira muda wote basi atachapika maana France wanao watu wanaoweza kupiga pasi hatarishi zinazoweza kuvunja mstari wa ulinzi wa Morocco hasa Olise, licha ya kwamba anaweza kupata goli Kwa counter attacks....
Umejiwahi kuwa wewe ni mbaguzi, kisa wale ni waarabu umeamua kuwa upande wa nchi inayohalalisha upindeNawapa france kwa waafrika wenzangu waliopo ulaya
potelea mbali niitwe mbaguzi!
Kwahiyo unaamini waafrika tunabebwa leo?Inashangaza sana Marefa wote wa hii gemu ni kutoka Argentina.