FT: Ihefu SC 2-1 Young Africans SC | NBC Premier League | Highland Estates | 04/10/2023

FT: Ihefu SC 2-1 Young Africans SC | NBC Premier League | Highland Estates | 04/10/2023

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
[emoji471] #NBCPremierLeague
[emoji460]️ Ihefu SC Vs Young Africans SC
[emoji414] 04.10.2023
[emoji909] Highland Estates
[emoji797] 10:00 Jioni

Matokeo ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja huo msimu uliopita ambapo Ihefu iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ndio yanayoonekana kuchangia zaidi kuongeza msisimko wa mechi hiyo ya leo kwani yaliifanya Ihefu kuizuia Yanga kuweka rekodi ya kucheza mechi 49 za Ligi Kuu bila kupoteza.

Yanga inaingia katika mechi ya leo ikiwa na historia ya ubabe dhidi ya Ihefu kwani zimekutana mara nne kwenye Ligi Kuu, ikipoteza mechi moja na kuibuka na ushindi katika michezo mitatu.

Mbali na hilo, mabingwa hao watetezi wanaonekana kuwa na mwanzo mzuri katika ligi kuu msimu huu ambapo wameibuka na ushindi katika mechi zao zote tatu zilizopita dhidi ya KMC, JKT Tanzania na Namungo FC, huku wakifunga mabao 11 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili tu.

Ni tofauti na Ihefu ambayo katika michezo mitatu iliyopita, imepata ushindi mara moja tu na kupoteza mechi mbili, ikifunga bao moja na yenyewe imefungwa mabao mawili.

Tukutane muda huo.

Inaweza kuwa mechi ya Kisasi.

View attachment 2771681View attachment 2771682
 
[emoji471] #NBCPremierLeague
[emoji460]️ Ihefu SC Vs Young Africans SC
[emoji414] 04.10.2023
[emoji909] Highland Estates
[emoji797] 10:00 Jioni

Tukutane muda huo.

Inaweza kuwa mechi ya Kisasi.
Mh natamani kuona highland panakuwa pachungu .

Natamani mkung'utwe ila kila nikiwangalia IEFU naona hakuna sababu ya mimi kuamini upuuzi wa namna hiyo katika umri huu niliyonao .

By the way kila la kheri mtani.
 
Menenene tekeri na peresi, maana yake ufalme wako umepimwa kwa mizani, nao umeonekana umeshindikana
 
Menenene tekeri na peresi, maana yake ufalme wako umepimwa kwa mizani, nao umeonekana umeshindikana
Ni bora ningeyaishi haya ya jina langu maana pombe na wanawake vimenitoa kwenye kijana smart mpaka kijana wa ovyo .

Nipo zangu kazini hapa , wagonjwa wamegoma kutibiwa na mimi , nimeamua kukaa tu nisubiri muda wa kutoka nisign out nikawaangalie Yanga tu .[emoji24]
 
Unamaanisha au maana kuna Dr mmoja pale Dodoma yupo kwa hali hiyo aisee muda wote ni kutetemeka tu na ni bado kijana mdogo
 
[emoji471] #NBCPremierLeague
[emoji460]️ Ihefu SC Vs Young Africans SC
[emoji414] 04.10.2023
[emoji909] Highland Estates
[emoji797] 10:00 Jioni

Tukutane muda huo.

Inaweza kuwa mechi ya Kisasi.
Kwann sikuhizi mnaanzisha nyuzi kama mnakimbizwa kaa Chini chambua andika Uzi wa mechi unaovutia... Mnakera aisee... Anyway all the best champion Dar Young Africans
[emoji169][emoji172]
 
Back
Top Bottom