FT: JKT Tanzania 0-0 Yanga | Meja Generali Isamuhyo stadium | Ligi kuu NBC | 10.2.2025

FT: JKT Tanzania 0-0 Yanga | Meja Generali Isamuhyo stadium | Ligi kuu NBC | 10.2.2025

Usiwaonee wivu wenzako. Timu yako ya simba imezipokea hizo pesa mara 4 mfululizo, mbona husemi? Na Mwezi ujao utashangaa mnazipokea tena! Ila kwa JKT, roho inakuuma eti!
NARUDIA TENA LABDA JKT WAZIKATAE HELA ZA YANGA KINYUME NA HAPO WATAFUNGWA TU.

MC ALGER,TABORA,AZAM NA AL HILAL WALIZAKATAA HELA ZA YANGA MAMBO YAKAWA MAGUMU.
 
Tunafaam kipa wa JKT umeambiwa usikaze dirisha kubwa watakusajiri tunakuomba usiingie kwenye huo mtego yanga ni matapeli kweli kweli
 
HII MECHI YANGA ATASHINDA TU LABDA JKT WAKATAE HELA ZA YANGA WAAMUE KUCHEZA MPIRA.

LEO JKT WATACHEZA HOVYO HATA PASI MBILI HAWATAPIGA NA WATAFUNGWA 3 AU 4 ILA WANGEKUWA WANACHEZA NA SIMBA MOTO UNGEWAKA WANGEJITUMA MPAKA WAFIE UWANJANI.
Ukisikia gubu la mke mwenza ndio hili sasa
 
Matokeo ya leo ni 1-4
IMG_20210715_175055_302.jpg
 
Mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu ya NBC, Yanga leo wako uwanjani Meja Jenerali Isamuhyo kumenyana na JKT Tanzania katika mechi ya raundi ya 18

Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kuzisaka alama tatu ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi

Itakuwa mechi rasmi ya kwanza kwa kocha Miloud Hamdi ambaye alijiunga na Yanga Jumatano iliyopita akichukua mikoba iliyoachwa na Sead Ramovic aliyetimkia Algeria

Leo Yanga itakuwa inasaka ushindi wa kwanza katika uwanja wa Isamuhyo.Wananchi wana kumbukumbu ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana katika uwanja huo msimu uliopita

Hata hivyo dimba la Isamuhyo kwa sasa ni bora na linaruhusu mpira kutembea tofauti na msimu uliopita ambapo mechi iliahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kupigwa siku iliyofuata katika uwanja uliokuwa umejaa tope

Hamdi ameahidi kuendeleza pale alipoishia Ramovic huku akiweka wazi chini yake Yanga itakuwa ikishambulia zaidi ili kufunga mabao mengi

Usikose kuitazama mechi hii LIVE kupitia simu yako download app hii itakayokuwezesha kuitazama mechi live BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP
 
Kila la kheri wananchi.
Japo maadui ni wengi ushindi mkubwa bado unawezekana.
 
Back
Top Bottom