Mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu ya NBC, Yanga leo wako uwanjani Meja Jenerali Isamuhyo kumenyana na JKT Tanzania katika mechi ya raundi ya 18
Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kuzisaka alama tatu ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Itakuwa mechi rasmi ya kwanza kwa kocha Miloud Hamdi ambaye alijiunga na Yanga Jumatano iliyopita akichukua mikoba iliyoachwa na Sead Ramovic aliyetimkia Algeria
Leo Yanga itakuwa inasaka ushindi wa kwanza katika uwanja wa Isamuhyo.Wananchi wana kumbukumbu ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana katika uwanja huo msimu uliopita
Hata hivyo dimba la Isamuhyo kwa sasa ni bora na linaruhusu mpira kutembea tofauti na msimu uliopita ambapo mechi iliahirish