FT: Jwaneng Galaxy 0 - 0 Simba | CAFCL | Francistown Stadium | 02.12.2023

FT: Jwaneng Galaxy 0 - 0 Simba | CAFCL | Francistown Stadium | 02.12.2023

Ni moja wapo ya timu ambayo kwa mtazamo wangu haikustahili kufika hapa ilipo, na imefika hapa kutokana na uzembe walioufanya Orlando Pirates.... kwenye preliminary stage Ile game ya kwanza Pirates eti walipunzisha wachezaji wao muhimu sababu ya game ya Ligi iliyokuwa mbele yao dhidi ya Sundowns, matokeo yake wakafungwa, halafu game ya pili majamaa yaka watoa kwa matuta.

Imagine sasa hivi tungekuwa tunaangalia mechi ya Simba vs Pirates na sio hawa washamba wanaotegema kubaki basi tu na kufunga magoli ya kuvizia vizia.
Mie nawaona hawana kabisa ile quality ya champions league.
 
Wapewe pongezi zao tu sababu timu inayoatahili kuvuka ni ile inayokusanya point na wamefanya hivyo halafu wanaendelea kufanya.
Pongezi wanastahili tu kama formality lakini sio pongezi za dhati.

Unafikiri ni kwanini Diego Somione pamoja na kuifikisha Atletico Madrid hapo ilipo Leo hii, lakini dunia haimuimbi? Na hayumo hata kwenye orodha ya makocha 10 Bora barani ulaya?

Na pia unadhani ni kwanini dunia inamuongelea sana Roberto De zarbi na wakati ni kocha wa juzi tu hapa??

Football ni zaidi ya kukusanya points na Kisha kuvuka hatua inayofuata mzee
 
Unafinya mara mia tano ya nini sasa? Baleke katukosea hajawa serious pale.
 
Mpaka sasa Simba haijashinda mechi yeyote ya kimataifa ndani ya huu msimu.

Msimu huu neno 'ushindi' umegeka msamiati mgumu kwa Mnyama.
 
Back
Top Bottom