FT: Jwaneng Galaxy 0 Simba SC 2

FT: Jwaneng Galaxy 0 Simba SC 2

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Ni siku kubwaaa, Siku Yenye Msisimuko Wake, Siku Ya Furaha Kwa Wapenzi wa Soka Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika Ya Kati na Afrika Kwa Ujumla. Ni mchezo wa Kuwania Kufuzu Hatua Makundi Club Bingwa Afrika ni kati ya Miamba Ya Soka Ya Botswana Jwaneng Galaxy Na Miamba ya Soka Tanzania Bara, Simba Sport Club. Ni mida ya Saa 9 alasiri Kwa Saa Za Botswana na Ni Saa 10 Jioni kwa Saa Za Tanzania, Macho, Masikio na Mikono Yako Viwe pamoja Nasi Hapa Kwenye jukwaa La Michezo Jamii Forum katika Uzi Wa Kuhabarishana Live kinachoendelea Kati ya Jwaneng Galaxy Na Simba Sc.

Bashasha, Shangwe, Furaha na Msisimuko wa Mechi Hiii unakuja Baada Ya Watani wa Jadi wa Simba Sc nikizungumzia Young Africans Kutolewa Hatua za Mwanzo Kabisa Kwa Kufungwa Nje Ndani Katika Hatua Ya Mtoano ya Club Bingwa Afrika na Rivers United watoto wa Nigeria. Wapenzi wa Soka Wanajiuliza Je, Na Simba Sc Itatolewa hatua Za Mwanzo? Au itapambana kiume kuendelea na Record Yake ya Club Bingwa Afrika?

Simba Sc Inarudi kwenye Michuano Ya Club Bingwa Afrika Ikiwakosa Nyota Wake wa 2 mahili ambao ni Triple C na Kijana wa Msumbiji Konde Boy, Luis M. Je Simba Inakwenda Kutoenesha Nini Siku Ya Leo? Tuwe hapa Wote kwa Dakika 90 za Mchezo huu

JWANENG GALAXY
Jwaneng Galaxy Ni Club iliyopo nchini Botswana ikipatikana mitaa ya Jwaneng na ikishiriki ligi kuu soka nchini Botswana. Botswana hupenda kuwaita Galaxy, Timu ilianzishwa Mwaka 2014, na Mwaka 2015 Timu mbili ziliungana na Kutoa JWANENG GALAXY CLUB, Timu hizi zikiwa ni The Jwaneng Comets na The Debswana Youngsters. Na Mwaka Huo Huo 2015 Jwaneng Galaxy Walishinda Taji la First Division South, Wanatumia Uwanja wao ujilikanao kama Galaxy Stadium wenye uwezi wa Kuchukua Mashabiki 2,000 na Kocha Wao Anaitwa Miguel da Costa, Msimu wa 2019/2020 Jwaneng Galaxy Walifanikiwa kumaliza legue Ya Botswana wakiwa nafasi ya kwanza na Kuchukua Ubingwa baada ya League Ya Botswana Kusimamishwa kwasababu ya COVID-19 Wakiwa na Point 41 mbele ya Township Rollers waliokuaa na Point 40. Jezi zao za Nyumbani ni Nyekundu na Nyeupe na Jezi zao za Ugenini ni Blue Na Nyeupe.

Msimu wa Mwaka 2016/2017 Jwaneng Galaxy Club Chini ya Kocha Mzambia Bwana Mike Sithole, Jwaneng Galaxy walifanikiaa kushinda Taji la club's first silverware lijulikanalo kama the Mascom Top 8 Cup, kwa kuwafunga Orapa United Kwenye extra time katika Fainali. Mwaka huo huo wakamaliza Nafasi ya Pili katika Ligii kuu Nchini Bitswana Na Kufanikiwa kufuzu kucheza CAF confederation Cup Mwaka 2018

Novembef 2017 Jwaneng Galax Waliamua Kumtimua Kocha Mzambia Bwana Sitole na Kuendelea kusalia nafasi ya pili msimu wa 2017/2018 nchini Botswana wakiwa nyuma kwa Point 4 Dhidi ya Vinara wa Ligii kuu Nchini Botswana Township Rollers F.C. Mwaka 2018/2019 Miguel da Costa akaajiriwa kama Kocha Mkuu kwa Msimu Wa 2018/2019 akitokea nchini Uaganda kwenye club ya Uganda's Vipers SC.

Jwaneng Galaxy Wameshiriki Michuano ya Shirikisho Club Bingwa Afrika mara Mbili, Mwaka 2018 Wakifungwa Nje ndani Na club ya Msumbiji CD Costa do Sol Kwa Jumla ya magoli 2.

Hii ni Mara Ya Pili Wanashiriki Michuano Ya Club Bingwa Afrika Hatua Ya Mtoano Baada ya Mwanzoni mwa Mwaka 2021 kutolewa na Mamelod Sundowns Kwajumla Ya Magoli 5 Kwa 1 wakifungwa Goli 3 kwa 1 wakiwa ugenini Kwa Madiba December 2020 Na Goli 2 kwa 0 wakiwa Nyumbani Bostwana, January 2021. Katika Hatua Ya Awali ya Mtoano. Na Kurudi kwenye Michuano Ya Shirikisho Afrika Ambako Walitolewa na Orando Pirates ya South afrika Wakifungwa Jumla ya Goli 4 mwezi February,2021 Goli 3 kwa 0 Wakiwa Nyumbani Na Goli 1 kwa 0 wakiwa Ugenini.

Mwaka Huu Wanakutana na Simba Baada ya Kufuzu hatua ya Pili Kwa Tofauti ya Magoli baada ya Kucheza na Diplomates na Kuwafunga Goli 2 kwa 0 wakiwa nyumbani Botswana, Na kufungwa Goli 1 kwa 0 wakiwa Ugenini wakicheza na Diplomates katika hatua ya Marudiano Mwezi wa 9 mwaka Huu

Leo Hii October 17, Wanakutana Na Simba Sc, Je Nini Kitatokea?

Here We Go
 
Leo mikia wanatoa hela, weka hela kwa mwenyeji, upige pesa kiulainiii
 
Back
Top Bottom