FT: Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC | Klabu Bingwa Afrika CAFCL | FNB Stadium

FT: Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC | Klabu Bingwa Afrika CAFCL | FNB Stadium

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Timu mbili kutoka Nchi marafiki, Afrika Kusini na Tanzania zinakutana leo Jumamosi ya Mei 15, 2021 kwenye uwanja wa kwanza Afrika kuchezwa fainali za Kombe la Dunia, ambapo Kaizer Chiefs wanakabiliana na Simba SC katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa FNB Stadium nchini Afrika Kusini.

Mchezo inatarajiwa kuwa mkali na wa vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika 90, mchezo ambao utachezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani.

Kaizer Chiefs wakiwa nyumbani katika hatua ya makundi hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye uwanja wa FNB, wameshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja huku wakiwa hawajaruhusu bao kwenye michezo yote mitatu.

Simba SC ushindi wa michezo minne na sare ya mchezo mmoja huku ikiwa wamepoteza mchezo mmoja na kujikusanyia alama 13 na kumaliza vinara wa kundi A wanakipiga na Kaizer Chiefs wakiwa wameshika nafasi ya pili kwenye kundi C kwa alama 9.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 kwa saa za Tanzania na saa 12:00 kwa saa za Afrika Kusini.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

Kaizer Chiefs Vs Simba SC

===============

00' Mpira umeanza dimba la FNB

04' Almanusura Kaizer waandike goli la kwanza baada ya Manya kubaki na goli lakini akajigonga, kona.

05' Goooooooooaaal Kaizer Chiefs wanatangulia kwa bao la kwanza kupitia kwa Erick Mothoho, mpira ulioanzia kwenye kona. Kaizer Chiefs 1-0 Simba SC

11' Chris Mugalu ansshindwa kuipatia Simba SC bao, baada kushindwa kumalizika pasi ya Miquissone

Simba wametulia sasa wanacheza kwa kupasiana kujaribu kupenya ngome ya Kaizer Chiefs.

Cardoso ansshindwa kufunga bao, kufuatia mpira wa Free Kick iliyopigwa.

Miquissone anafanyiwa madhambi nje kidogo ya 18 ni faulo kuelekea Kaizer, Inapigwa, mpira unababatiza ukuta wa Kaizer

33' Goooooooooaaal Kaizer Chiefs wanaandika bao la pili kupitia kwa Nurkovic, mpira wa kichwa. Kaizer Chiefs 2-0 Simba SC

40' Chama anakosa nafasi ya wazi kuweza kusawazisha, baada ya mpira kutoka Sentimita chache ya goli, ilikuwa pande maridadi kutoka kwa Miquissone

45' CAFCC, mpira ni mapumziko ambapo Kaizer wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila

HT, CAFCL; Kaizer Chiefs 2-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa FNB, huku umiliki wa mpira ni kwa Simba sasa, tuone mambo yatakuwaje

Goooooooooaaal Nurkovic anaipatia Kaizer Chiefs bao la tatu kwa shuti.. Kaizer Chiefs 3-0 Simba SC

Goooooooooaaal Kaizer Chiefs bao la nne, makosa ya mabeki yanazidi kuigharibu timu. Kwakweli mpira ni mgumu upande wa Simba, Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC

90+3' Matumaini ya kupata walau bao moja la kufutia machozi yanazidi kufifia FNB Stadium

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Kaizer Chiefs wameibuka na ushindi wa mabao manne kwa bila dhidi ya Simba SC.

FT, CAFCL; Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC

....Ghazwat
 
Hivi kwa nini wasauzi walibadilisha jina la hicho kiwanja cha mpira kutoka soccer city kwenda fnb? Mana jina la soccer city lilikuwa limebamba kweli kipindi hicho cha world cup 2010.
 
Balozi wa uingereza anawakubali wasimbazi.
Screenshot_20210515-141303.jpg
IMG_20210515_141718.jpg
 
Vipi Azam washasogea huko bondeni kutuonyesha mpira au dau wamelishindwa tena kama mechi ya Plateau
 
Back
Top Bottom