Kosa la kwanza ni lenu wenyewe. Kwa nini wiki mbili anakaa bila kucheza mechinya ushindani? Mlitakiwa kucheza mechi ya coastal union.
Pili ni kwamba hii level mnakutananna makocha wanaofundisha na sio kusimamia mazoezi au kuhasisha. Game plan ya chiefs ilikuwa sport on. Kocha wenu kashindwa kabisa kung'amua jinsi ya kucheza dhidi ya 5-2-3 formation. Yani mpaka boko anaonekana kumwambia kocha... bwana mkubwa pale mugalu anakabwa na wachezaji watatu.
Sasa hiki ni kitu ambacho kunakuja moja kwa moja kwenye ligi yetu. Huku kwetu sie ni 4-4-2 tuu hamna variation za formations hivyo basi wachezaji wanakuwa hawajapitia changamoto za kukabiliana na mifumo tofauti. Tunadanganyaga kuwa oh mfumo hauchezi. Huo ni kutokujia mpira.
Jinsi unavyo shambulia dhidi ya back 5 na back 4 ninvitu viwili tofauti. Kunancertain patterns ambazo haziwezi kuwa effective against a back 5. Na ndicho kilichowakuta simba leo.
Kwa wenzetu huko wanaojua mpira. Wachezaji wanafundisha jinsi ya kukabiliana na different formations. Ata barca pamoja na kuamini mfumo wa 4-3-3 bado wanafundisha mifumo mingine na jinsi ya kuikabili.
Long story short...hunt won the tactical battle today.