Ukiwa broke utaona kupewa 100 ni bonge ya love.
Lakini kwa tajiri hiyo ni dharau.
Mtu ambaye anapata 1.5B kwenye michuano migumu ambayo sio rahisi wewe mwenye 500M ya NBC kuipata, utasemaje mwenye 500M ameheshimika?
Utaona ni heshima kwasababu ya umasikini wako, na ndio maana kila zinapotolewa rank za timu bora Africa haujawahi kutajwa licha ya kwamba una heshima ya kombe la NBC.
Mashindano makubwa hapa Afrika ni Club Bingwa tu.
Yeyote anayefanya vizuri kwenye hii michuano ndio mwenye nafasi kubwa ya kujimilikisha heshima.
Ni kweli mshindi wa confederation anachukua pesa nyingi kidogo kumzidi yule aliyefika robo ya Club Bingwa.
Lakini we jiulize, kwanini kuna gape dogo kwenye hiyo pesa kati ya mshindi wa federation na aliyetolewa kwenye robo ya Club Bingwa?
Maana yake ni kwamba huyu wa Club Bingwa akiwa katika hatua za chini anakuwa amefanya kazi kubwa sana ambayo ili kuilinganisha na level za confederation basi ni mpaka uongeze level mbili au tatu za juu ndio upate ratio sawa.