Kama si Mbiringe bila shaka ni Patashika ya Ligi Kuu Tanzani Bara [emoji1241] kuendelea kupigwa leo Jumatano ya Novemba 16, 2022 kwa Mnyama Mkali Mwituni Simba SC [emoji881] kukiwasha vilivyo na Wababe wa Kusini Namungo FC, katika Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam [emoji2522]
Mchezo unatarajiwa kuwa ngumu kwa pande zote mbili kulingana na maandalizi na ubora wa vikosi vyao huku makocha wote wakisema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo. Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi ya mchezo yapo vizuri.
"Kwa ujumla ni kwamba maandalizi ya mchezo wa leo yanakwenda vizuri, kwa maana kuwa tupo tayari kucheza mchezo wetu na mpinzani wetu kutoka Lindi". alisema Kocha Mgunda.
Naye Kocha Msaidizi wa Namungo FC Shadrack Nsajigwa kuelekea kwenye mchezo huo amesema kuwa wamejiandaa kushindana na Simba SC.
"Kimsingi tumekuja kushindana na Simba SC, tumepata muda wa kujiandaa kiasi cha siku 8 kwahivyo timu yetu ipo tayari kwa ajili ya kushindana na Simba SC". amesema Kocha Shadrack.
Tutegemee kuona ushindani wa kweli ndani ya dakika 90 za jasho na damu kutoka pande zote mbili katika kugombea alama tatu muhimu za Ligi Kuu Tanzania Bara..[emoji288]Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1;00[emoji354] Usiku.. Usikose Ukaadithiwa Yaani.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.[emoji2424][/B]