Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa, mimi ni mshabiki wa Azam 👍🏾👍🏾👍🏾Tushawakanda
Hata huko tanesco wamepita na umeme wao 😂😂JamiiForums hakuna umeme au?
Wekeni uzi live acheni hizo nyie
Haya endelea kutupatia updates sasaSisi 1 wao 0.
Weekend hii lazima niwe kwenye bar kubwa yenye jenereta la uhakika
Hawa tanesco sijui wana maana gani,siku nzima umeme upo mpira unakaribia wanachukuaTanesco washachukua chao
Hawa wa kubebwa hawaishiwi tu penalties !View attachment 2892593
All the Best Mnyama mkali.
Tukutane saa 10jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)
Simba ya Dar es Salaam itashuka Dimbani, Uwanja wa Ziwa Tanganyika kuwavaa wenyeji wao Mashujaa FC.
Simba kwenye msimamo wa Ligi yuko nafasi ya 3. Amecheza michezo 10.
Akiwa na Alama 23. Anayeongoza ligi Azam FC ana michezo 13 na Alama 31.
Simba anaingia kwenye mchezo huu wa 11 akiwa na hasira baada ya kutoa suluhu na KMC mchezo wake wa ligi uliopita.
Mashujaa wao wako Nafasi ya 15 out of 16. wakiwa na alama 9 tu kwa michezo 12.
#nguvumoja#
Kikosi cha Mashujaa Kinachoanza.
View attachment 2892932
Kikosi cha Simba Kinachoanza
View attachment 2892924
Updates...
Lake Tanganyika imefurika,
Mashabiki ni wengi sana
Timu ndio zinaingia uwanjani.
Tuwe pamoja nitawajuza matukio yote muhimu kwenye hii game.
Tuwe sote,
Uran....
Dakika 0:40'
Mpira umeonekana kama hauna upepo ukabadilishwa
Dakika 4'
Mpira unaendelea inaonekana bado Simba hawajakaa vizuri.
Mpira uko upande wao sana.
Dakika 7'
Game on...
Mashujaa 0- 0 Simba.
Mpira umetulia bado hakuna mashambulizi makali kutoka pande zote.
Dakika 9'
Fred anakosa goli la wazi kabisa.
Baada yakutokea shambulizi kali kwenye lango la Mashujaa.
Dakika 13'
Simba wanapata penalti.
Ni penalty ya wazi kabisa.
Kibu D amefanyiwa madhambi ndani ya boxi la Mashujaa.
Ngoja tuone.
Dakika 16'
Goaaaaaaaaalllll
Simba wanapata goli la kuongoza kupitia mkwaju wa Penalti.
Anafunga Saidoo Ntibazonkiza.
Dakika 17'
Manula anaokoa shambulizi la mashujaa.
Game on...
Mashujaa 0-1 Simba
Dakika 24'
Game on...
Simba wanafanya mashambulizi yakushtukiza kwenye lango la Mashujaa.
Kanoute yuko chini mpira umesimama kidogo.
Anafanyiwa matibabu.
Dakika 27'
Mpira unaendelea.
Mashujaa 0-1 Simba
Dakika 29'
Simba wanapata kona, inapigwa inakuwa tasa.
Dakika 31'
Simba wanafanya shambulizi kali, Saido anapiga kick nyepesi sana inaishia kwenye mikono ya Kipa.
Dakika 37'
Kibu anaonekana kutumia akili zaidi kwenye lango la Mashujaa.
Free Kick.
Nje kidogo ya Mashujaa.
Saidoo anapiga inakuwa goal kick.
Umeme wenyewe tunaulipia halafu wanaukata, wapumbavu wakubwa, yaani wao na Waziri wao wa nishati ni wapumbavu kabisaHawa tanesco sijui wana maana gani,siku nzima umeme upo mpira unakaribia wanachukua
Sent using Jamii Forums mobile app
Itakuwa pitch ina visikiBado SIMBA ina- strugle namna ya kutengeneza CHANCES..
MZAMIRU, KONOUTE na SAIDOO wote wanakimbia wakiwa wanaangalia chini