View attachment 3664237
MATCH DAY.
Leo Septemba 6, 2026, Simba SC inatupa karata yake ya kwanza ya CAF Champions League ugenini dhidi ya Mighty Wanderers pale Bingu National Stadium, Lilongwe, Malawi (Muda: Saa 10:00 Jioni EAT).
Hali ya Simba SC: Inaingia ikiwa na morali ya ushindi wa mechi 5 mfululizo kwenye Ligi Kuu (NBC). Changamoto pekee ni kukosekana kwa mabeki Shomari Kapombe na Nickson Kibabage, lakini uzoefu wa kimataifa wa kikosi na uwepo wa mafundi kama Clatous Chama unampa Mnyama nafasi kubwa.
Mighty Wanderers: Wakiwa nyumbani wanajua fika kuwa lazima wapate ushindi ili kujiweka salama kabla ya kuja Dar es Salaam kwenye marudiano Watacheza kwa nguvu na kushambulia kwa kushitukiza.
Simba atashinda hii game.
#nguvumoja.
Kikosi cha Simba.
View attachment 3664411
Tukutane saa 10 kwa Updates...