FT: NBCPL, Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar | Uwanja wa Mkapa | 30/10/2022

FT: NBCPL, Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar | Uwanja wa Mkapa | 30/10/2022

kileleni kuna baridi kali, huko chini naona mnajipongeza na magoli tu
JamiiForums-1696028063.gif
 
Tumeshinda ila kadi mbili na goli kipa wa mtibwa sugar imeifanya game kukosa ladha halisi na ushindani.
 
Augustine Okrah ni mchezaji pekee ambaye akijua amekosea humuoni tena akirudia makosa yale yale

Tangu mechi ya Derby amekuwa ni mchezaji mwenye utulivu wa hali ya juu na kutoa pande kwa wenzake pale inapo hitajika

Mzamiru Yassin leo amekiwasha ukiachana na kufunga goli pia katoa na assist, the same kwa Okrah

Ila kiwango chake leo Mzamiru kilikuwa kizuri sana

Kapombe nilitegemea kumuona akiwa slow kutokana na majeraha yaliyomuweka ndani kipindi kirefu, lakini mashambulizi mengi yametengenezwa kupitia upande wake.

Chama sio wa kumzungumzia sana maana yake huyu shughuli yake inajulikana mpaka kwa haters ambao wanamfananisha na mchezaji wao.

Moses Scars Phiri ni mchezaji ambaye hachezi kwa faida yake, anacheza kwa ajili ya timu. Ni mchezaji bora mwenye mahesabu asiye na papara pindi apatapo mpira kwenye box.

Kongole kwake now ana goli 5

Sakho, ukiacha ile foul yake ambayo wadau wametoa maoni kuwa ilipaswa kuwa zaidi ya yellow card, lakini leo kaonesha kitu cha kiutofauti kidogo ukilinganisha na mechi zake mbili zilizopita.

Sijajua kama ubora huu aliokuwa nao leo umetokana na weakness ya Mtibwa kupungukiwa na wachezaji wawili. Ila nilianza kumuangalia mapema kabla ya kadi nyekundu hazijatolewa, alikuwa superb.
 
Redi kadi zimeamua matokeo ya kipuuz,kariaaaa na tumbo lake kafurahi sana leo
Hata kipa pia hajawahi kucheza mechi yoyote ya premier league msimu huu mmoja yupo Tanzania under 20 mwingine mgonjwa hvyo kipa hakuwa sawa kwenye mechi ya leo
 
Kuna haja ya kuwa na msimamo wa ligi wa kweli. Kiuhalisi Utopolo haitakiwi iwe kileleni, ina points 15... wana points 3 za kupewa za Azam (mpira ulitoka nje) na point 2 za bure za Geita Gold
Acha kuwa kama bumunda
 
Yanga wanashangaa Mtibwa kufungwa Mkono...wakati wao tulishawafunga hivyo..au wazee wa historia wamesahau
 
Yanga wanashangaa Mtibwa kufungwa Mkono...wakati wao tulishawafunga hivyo..au wazee wa historia wamesahau

Mikia ilipigwa kipogo cha mbwa mwitu kipindi cha pili haikurudi uwanjani au umejisahaurisha!!!!?
 
mikia ilipigwa kipogo cha mbwa mwitu kipindi cha pili haikurudi uwanjani au umejisahaurisha!!!!?
Ujinga kujitwisha ujinga. Mechi ilikuwa 0 kwa 0 hadi mapumziko kipindi cha pili Simba hawakurudi. Utopolo kapewa ushindi wa mezani point 2 na magoli 2.

Labda hizo goli 2 za mezani ndio kipigo unachobweka
 
Back
Top Bottom