Augustine Okrah ni mchezaji pekee ambaye akijua amekosea humuoni tena akirudia makosa yale yale
Tangu mechi ya Derby amekuwa ni mchezaji mwenye utulivu wa hali ya juu na kutoa pande kwa wenzake pale inapo hitajika
Mzamiru Yassin leo amekiwasha ukiachana na kufunga goli pia katoa na assist, the same kwa Okrah
Ila kiwango chake leo Mzamiru kilikuwa kizuri sana
Kapombe nilitegemea kumuona akiwa slow kutokana na majeraha yaliyomuweka ndani kipindi kirefu, lakini mashambulizi mengi yametengenezwa kupitia upande wake.
Chama sio wa kumzungumzia sana maana yake huyu shughuli yake inajulikana mpaka kwa haters ambao wanamfananisha na mchezaji wao.
Moses Scars Phiri ni mchezaji ambaye hachezi kwa faida yake, anacheza kwa ajili ya timu. Ni mchezaji bora mwenye mahesabu asiye na papara pindi apatapo mpira kwenye box.
Kongole kwake now ana goli 5
Sakho, ukiacha ile foul yake ambayo wadau wametoa maoni kuwa ilipaswa kuwa zaidi ya yellow card, lakini leo kaonesha kitu cha kiutofauti kidogo ukilinganisha na mechi zake mbili zilizopita.
Sijajua kama ubora huu aliokuwa nao leo umetokana na weakness ya Mtibwa kupungukiwa na wachezaji wawili. Ila nilianza kumuangalia mapema kabla ya kadi nyekundu hazijatolewa, alikuwa superb.