FT: Nusu Fainali ASFC Cup: Azam FC 2-1 Simba SC : 07-05-2023, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara

FT: Nusu Fainali ASFC Cup: Azam FC 2-1 Simba SC : 07-05-2023, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara

[emoji1787][emoji1787]
20230507_180720.jpg
 
Mpaka Sasa mwekezaji amesema ameshatumia bilioni 55 ukiacha zile bilioni 20 za uwekezaji.
Pesa zote izo timu inaishia robo ya Caf champion league na bado anatakiwa atie mzigo Ili timu iweze kuvuka robo.
Kama Mo hatutapeli basi yeye katapeliwa,kama hajatapeliwa basi kutakuwa na watu wapumbavu kuwahi kutokea kuongoza soka kiasi cha kutumia pesa zote hizo na huchukui kikombe chochote!

Utopolo wametumia kiasi kisichozidi b. 15 na ndio wapo hapo!

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
KILA SIKU TUNAWAAMBIA ACHENI KULETA WACHEZAJI MIZIGO. TIMU INATAKIWA IFANYE MABADIRIKO. VIONGOZI WANAPASWA WAJIUZURU NA WACHEZAJI WAONDOSHWE.

Kwanini mmepoteza Beno kakolanya kirahisi hivyo????


1. Mohamed Ottara.
2. Joash Onyango.
3. Ismail sawadogo.
4.Peter Banda.
5. Pape Sackho.
6.Agustine Okrah.

WACHEZAJI WAZAWA WA KUACHWA.

1.John Boko.
2.Jonas Mkude.
3. GADIEL Michael.
4. Nassor Kapama.
5.Habib Kyombo.

NAFASI MUHIMU ZA KUJAZA.

1.Golikipa nambari Mbili.
2. Beki wa kushoto.
3. Mabeki wa kati .
4. Kiungo mkabaji ,, 6 ,, 8.
5. Mshambuliaji wa KIGENI futi sita.
6. Winga wa kushoto.

ZINGATIENI SANA VIMO VYA WACHEZAJI WALAU 6 FEET.

BORA KUSAJILI WACHEZAJI WACHACHE KULIKO KUWA NA RUNDO LA WACHEZAJI MIZIGO.
MOHAMED DEWJI.
TRY AGAIN.
MANGUNGO.
BODI YA WAKURUGENZI.
 
Nilimuangalia CHAMA mechi 3 mfululizo ( derby, Wydad- dar + Morroco.
Ni kama amechoka kimwili. Nadhani alitumika mfululizo sana..
Mechi KUBWA kama ya leo alihitaji kuanzia benchi..( si kwamba ni mbaya , ila alihitaji kupumzika..
Nadhani kocha alihofia pressure ya washabiki ambavyo hali aliikuta... Ila nashangaa kutotumika kwa phiri..
Ila kwa yote simba ilitumia energy nyingi ....i kama SIMBA players wamekuwa demoralized na matokeo ya ACL....
Chama akae nje alafu timu ifungwe! huyo kocha atapitia wapi?
 
Kama Mo hatutapeli basi yeye katapeliwa,kama hajatapeliwa basi kutakuwa na watu wapumbavu kuwahi kutokea kuongoza soka kiasi cha kutumia pesa zote hizo na huchukui kikombe chochote!

Utopolo wametumia kiasi kisichozidi b. 15 na ndio wapo hapo!

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Mkuu samahani sana, umesema uongo!

Unasema Thimba hajachukua kikombe chochote? Si kweli!

Thimba ana kombe la Mapinduzi moja, kombe la kuifunga Yanga la pili na makombe mawili ya kufa kiume moja dhidi ya Wydad na jingine dhidi ya Dube wa Azam Leo!
 
MZIZIMA DERBY

Ni mtanange wa kukata na shoka baina ya Azam Vs Simba katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho la Azam ndani ya dimba la NANGWANDA SIJAONA Mkoani Mtwara

Ni mchezo unaozikutanisha timu mbili zenye uhasama na mpira wa kiwango cha juu zaidi katika soka la Tanzania. Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana katika michuano hii ni msimu wa 2021 songea huko katika nusu fainali ambapo Simba ilishinda ushindi wa 1-0.

Azam itashuka dimbani ikihitaji kulipiza kisasi lakini pia kujaribu kutwaa ndoo hiyo huku Simba wakishuka dimbani kujaribu kushinda ili walau wapate taji la kufutia machozi msimu huu.

Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi wa mechi ya SINGIDA BIG STARS Vs YANGA katika mchezo wa Fainali utakaopigwa jijini TANGA baadae mwaka huu.

Huu ni mchezo ambao lazima mshindi apatikane. Hivyo hakutakuwa na droo.

Kutokana na uwanja wa NANGWANDA SIJAONA MTWARA kutokuwa na taa, mechi itapigwa saa 9:30 alasiri hivyo wapenzi na mashabiki mnakumbushwa kuwahi uwanjani na kwenye vibanda umiza.

Mchezo huu utakujia live kupitia Azam Sports 1HD na updates zote utazipata hapa usicheze mbali..
BAHLABANE BA NTWA


Mchezo umeanza
2' Simba wanapata faulo karibu na eneo la kona, Chama anapiga kipa anaokoa
10' Mchezo una kasi, timu zote zinapeana zamu kushambulia
12' Azam FC wanafanya shambulizi kali langoni kwa Simba, Zimbwe Jr anaokoa mpira uliokuwa unaelekea wavuni
13' Kibe Denis anaenda kushambulia lakini anacheza faulo
23' Gooooooooooal….
Azam FC wanatangulia kwa goli la Lusajo Mwaikenda baada ya kipa wa Simba, kuutema mpira ndani ya boksi
27' Goooooooooooal
Kanoute anasawazisha kwa kichwa kimalizia krosi ya Saido Ntibanzokinza
37’ Chama anachezewa faulo
40’ Mchezo unaendelea kwa kasi, wanapeana zamu kumiliki mpira
41’ Simba walianza kwa kasi ya chini, wanaongeza kasi muda unavyosogea
45’ Zinaongezwa dakika 2
45’ Chama anakosa nafasi akiwa yeye na kipa, shuti lake linaokolewa

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza

47’ Simba wanapata faulo, Chama anapiga nje
50’ Sopu nalalamika kuchezwa faulo ndani ya boksi
52’ Presha ya mchezo inaongezeka, Azam FC wanaonekana kutofurahishwa na maamuzi ya refa
53’ Azam FC wanafanya shambulizi kali
53’ Kibu Denis anakosa nafasi ya wazi akiwa yeye na kipa
73’ Bado mambo ni magumu, Azam FC ndio wanaofika langoni mwa Simba mara kadhaa
76’ Goooooooooooooooal
Prince Dube anafunga goli la pili kwa Azam FC
86' Kanoute anapata kadi ya pili ya njano, inakuwa nyekundu
90' Zinaongezwa dakika 4
90' + 4 Simba wanashindwa kupata goli la kusawazisha

FULL TIME
Bridger
 
Magoli alofungwa kipa wa Simba, angekuwa Yanga amecheza na timu nyingine angeshinda yale magoli, Simba wangesema huyo kipa kapewa bahasha.
Huyu kipa nilimtoa kwenye sehemu yake baada ya mechi ya Wydad
 
Back
Top Bottom